Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Msanii wa zamani wa kundi la Sailors, Shalkido, ameomba radhi hadharani kwa kumkosea heshima mchekeshaji maarufu Terence Creative, baada ya kumfananisha na mbwa katika kauli zake za awali. Akizungumza baada kulamba dili la ubalozi la Dignity Furniture, Shalkido amesema maneno hayo yalitokana na maumivu na changamoto alizokuwa akipitia, lakini amejitokeza wazi kuomba msamaha, akisisitiza kwamba anajutia matamshi yake na anaamini ni wakati wa kujenga heshima na mshikamano katika tasnia ya burudani. Kwa upande wake, Terence Creative amepokea msamaha huo kwa moyo wa upendo na akaahidi kuendelea kumuunga mkono kijana huyo, akisema kila mtu hupitia makosa na kinachohitajika ni kurekebisha mienendo. Juzi kati Shalkido alitangaza kuwa amefilisika kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya msingi. Hali hiyo ilisababisha Eric Omondi kujitokeza kumpa msaada wa pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya kimsingi, huku pia Wakenya wenye roho ya huruma wakikusanyika kuchanga pesa za kumsaidia kurejea kwenye hali yake ya kawaida

Read More
 Shalikido Afafanua Sababu za Kutoridhishwa na Ushauri wa Terence Creative

Shalikido Afafanua Sababu za Kutoridhishwa na Ushauri wa Terence Creative

Msanii wa Gengetone, Shalikido, amemkashifu mchekeshaji maarufu Terence Creative kwa kutoa ushauri kwa wasanii kuwekeza miradi mingine kando na muziki wakati anapitia changamoto kubwa za kifedha. Shalikido, ambaye hivi karibuni alijitokeza hadharani kuomba msaada wa kifedha, alisema ushauri wa Terence ulitolewa wakati usiofaa na haukuzingatia hali halisi ya matatizo aliyokuwa akikumbwa nayo. Alisisitiza kuwa mtu anapokumbwa na changamoto za kifedha, si rahisi kupokea ushauri wa namna hiyo bila kuelewa muktadha wa maisha yake na changamoto anazokabiliana nazo. Shalikido ameonyesha wazi kuwa badala ya kutoa maelekezo au ushauri usioeleweka, ni vyema kutoa msaada wa moja kwa moja au kuelewa hali ya mtu kabla ya kutoa mapendekezo. Kauli ya Shalikido imekuja siku chache baada ya Terence Creative kuwahimiza wasanii kupanga mikakati ya baadaye kwa kuwekeza katika miradi tofauti, akisisitiza kuwa maisha ya kuwa msanii si ya kudumu milele na kuwa kuna wakati uwezo wao wa kung’ara jukwaani utaisha.

Read More
 MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Member wa kundi la Sailors gang, Shalkido ametangaza kuachana kabisa na masuala ya muziki. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram,Shalikido amesema amechukua uamuzi huo baada ya kugundua kuwa muziki wake umepoteza mvuto kwenye jamii, hivyo ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee. “Baada ya muda mrefu kutafakari kuhusu kazi yangu ya muziki, nimegundua kuwa muziki wangu hauna mashiko.” “Kwa hivyo nimeamua kubadilisha kazi yangu kwa kufanya kitu kitakachoniridhisha zaidi maishani. Kwa mashabiki wangu wote walioniamini, samahani sana kuwaangusha.”, Ameandika kupitia instastory yake. Taarifa Shalkido kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya kutaka kusilikiza nyimbo za kundi la Sailors gang. Baadhi ya mashabiki wa shalkido wanahisi huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini ili aweze kuachia singo yake mpya.

Read More