Shatta Wale Akanusha Madai ya Kumtelekeza Mama Yake

Shatta Wale Akanusha Madai ya Kumtelekeza Mama Yake

Msanii wa muziki wa dancehall kutoka Ghana, Charles Nii Armah Mensah, maarufu kama Shatta Wale, amekanusha madai yanayosambaa kwamba amemtelekeza mama yake mzazi kwa kutompa mahitaji ya msingi. Akizungumza kupitia podcast ya moja kwa moja, Shatta Wale aliweka wazi kuwa amewahi kumsaidia mama yake kwa njia mbalimbali, ikiwemo kumpatia magari na makazi bora ya kuishi. “Huyo mama mnayemzungumzia… sidhani kama nyinyi mlishawahi kununulia mama zenu magari. Mimi nimeshanunulia mama yangu magari; nimefanya mambo mengi kwa ajili yake. Lakini katika maisha, kuna kushinda na kuna kushindwa.” alisema katika maelezo yake. Kauli hiyo inakuja kufuatia tuhuma zilizokuwa zinasambazwa mitandaoni na baadhi ya mashabiki wakidai kuwa msanii huyo mkubwa amemsahau mama yake licha ya mafanikio makubwa aliyoyapata katika muziki. Shatta Wale ameendelea kusisitiza kuwa anamheshimu na kumjali mama yake, na kwamba watu hawapaswi kuhukumu mambo ambayo hawana uhakika nayo.

Read More
 SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

Bifu la Shatta Wale wa Ghana na Burna Boy wa Nigeria linaendelea kushika kasi, Shatta Wale ameibuka na kuweka wazi kuwa yupo tayari kuingia ulingoni na African giant, Burna Boy. Kupitia mfululizo wa tweets za matusi katika mtandao wa Twitter  Shatta Wale alionekana mwenye hasira huku akitoa vitisho kwa Burna Boy asikanyaga kwenye ardhi ya Ghana kwani atamshushia kichapo cha mbwa kitakachoimuacha na majeraha. Shatta ametoa kauli hiyo mara baada ya Burna Boy kudai kuwa hatomvumilia msanii yeyote anayetaka kuigawanya tasnia ya muziki Afrika ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kuzichapa na Shatta Wale ambaye juzi kati amekuwa akiwashambulia mashabiki na wasanii wa Nigeria kwa kutosapoti muziki wa mataifa mengine ya Afrika. Hata hivyo Burna Boy hajajibu chochote mpaka sasa kuhusiana na ishu ya Shatta Wale kumtolea uvivu

Read More
 SHATTA WALE AMCHANA REMA KWA MADAI YA KUDHALALISHA WANAWAKE WA GHANA

SHATTA WALE AMCHANA REMA KWA MADAI YA KUDHALALISHA WANAWAKE WA GHANA

Siku chache baada ya kuwatolea uvivu mashabiki na wasanii kutoka Nigeria, mwanamuziki mkali wa dancehall kutoka Ghana Shatta Wale ,amemchana mwanamuziki kutoka Nigeria Rema kwa kile alichodai kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake wa Ghana. Hii ni baada ya Rema kupitia ukurasa wake wa Twitter kusema kwamba anataka wasichana 10 wa Ghana watulize akili yake kama njia ya kupunguza mawazo yake. Sasa akijibu tweet ya mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 21 Shatta Wale amemkashifu Rema kwa kuwadharau na kuwavunjia heshima wanawake wa Ghana.⁠⁣ Hivi karibuni mwanamuziki huyo mkubwa nchini Ghana alichukua headlines katika mitandao ya kijamii akidai kuwa wasanii na mashabiki wa Nigeria ni wabinafsi ikija suala la kusapoti muziki wa mataifa mengine.

Read More
 SHATTA WALE AWACHANA WANIGERIA KWA KUTOSAPOTI WASANII WA MATAIFA MENGNE

SHATTA WALE AWACHANA WANIGERIA KWA KUTOSAPOTI WASANII WA MATAIFA MENGNE

Mkali wa muziki wa dancehall kutoka Ghana Shatta Wale ameibuka kuwachana mashabiki wa muziki wa nigeria kwa kushindwa kutoa sapoti kwa muziki kutoka kwenye mataifa mengine. Shatta ametumia ukurasa wake wa twitter kutweet mfululizo wa tweets zinazo kosoa na kushambulia tabia alizo ziita ubinafsi za wasanii na mashabiki wa Nigeria. Lakini pia Shatta Wale ametolea mfano wa kile alichowahi kuzungumza mwanamuziki Mr Flavour akimtaja mwanamuziki aDiamond Platnumz kutoka Tanzania ni msanii mkubwa kwenye namba za mtandao wa YouTube kuliko wasanii wengi wa Nigeria lakini ni mara chache sana mashabiki nchini humo kumzungumzia ama kusapoti muziki wake.

Read More