SHEEBAH AFUNGUKA CHANZO CHA UCHAGUZI WA UMA KUAHIRISHWA

SHEEBAH AFUNGUKA CHANZO CHA UCHAGUZI WA UMA KUAHIRISHWA

Mwanamuziki Sheebah Karungi amefunguka sababu zilizopelekea uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA kuahirishwa. Kwenye mahojiano na Bukedde TV Sheebah amesema yeye ndiye aliwashawishi wasanii kususia upigaji kura kwa njia ya SMS kwenye uchaguzi huo ambao ulikumbwa na dosari. “Mimi nilichangia uchaguzi huo kufutwa, nilikuwa kwenye simu nikiwashawishi wadau mbalimbali kususia uchaguzi, nashukuru kamati ya uchaguzi ilisikiliza malilio yetu, sielewi ilikuwaje wafuasi wa King Saha washindwe kupiga kura kutokana na mtandao huo kuharibika na bado kura zote za Cindy zilikuwa zinaendelea kutiririka. Huo ulikuwa udanganyifu uliopitiliza,” alisema. Inadaiwa Sheebah ndiye anamfadhili kifedha King Saha kusambaratisha juhudi za Cindy Sanyu kutua uongozi wa chama cha wanamuziki nchini uganda kwa mara ya pili. Sheebah anajiunga na orodha ya wanamuziki kama Ykee Benda, Fefe Bussi, King Micheal, Spice Diana, Karole Kasita, Jose Chameleone, na Eddy Kenzo wanaoendelea kumshutumu Cindy Sanyu kwa kutumia vibaya pesa za wasanii kwa manufaa yake binafsi. Utakumbuka Uchaguzi wa UMA uliahirisha Juni 6 mara baada ya wafuasi wa King Saha kudai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi hadi sasa Kamati ya inayojishughulisha na uchaguzi hajatoa mweelekeo kama uchaguzi utarudiwa ila jambo la kusubiriwa.

Read More
 SHEEBAH KARUNGI AFUTA UTAMBULISHO WA TEAM NO SLEEP KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

SHEEBAH KARUNGI AFUTA UTAMBULISHO WA TEAM NO SLEEP KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Inaonekana Msanii nyota nchini Uganda Sheebah karungi anaendelea kujitenga na meneja wake wa zamani Jeff Kiwa. Taarifa mpya ni kwamba mrembo huyo amefuta utambulisho wa lebo ya Team No Sleep kwenye bio yake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Lakini pia amemuondoa Jeff Kiwa na mpenzi wake Mutoni Entana kwenye orodha ya watu anaowafuata kwenye mtandao wa instagram. Jeff kiwa na Sheebah hawajathibitisha rasmi kama wamevunja uhusiano wao ila wamekuwa wakitupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii. Ikumbukwe kwa sasa sheebah anaendesha shughuli zake za kibiashara kupitia kampuni yake ya Sheebah business limited huku jeff kiwa akiwa anapromote msanii wake mpya Rahmah Pinky.

Read More
 SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

Mwanamuziki wa lebo ya muziki ya Team No Sleep Sheebah Samali Karungi amefunguka na kusema kwamba ana mpango wa kuanzisha shule ya kutoa ujuzi wa kuwahamasisha watoto wa kike. Hitmaker huyo wa Yolo amesema lengo la yeye kuanzisha chuo hicho ni kuwaona wanawake wanaanza kujitegemea kiuchumi badala ya kukaa nyumbani wakisubiri waume zao wawape pesa na mahitaji ya msingi. Sheebah amedokeza kwamba ataendelea na mpango wake wa kutoa msaada kwa jamii maeneo yote nchini uganda kwa lengo la kuwahimiza watoto wa kike wajenge tabia ya kujitegemea katika maisha. Kauli ya Sheebah imekuja mara baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuanzisha chuo cha muziki ambacho kitakuza vipaji nchini uganda ili itoe  wasanii wenye tajriba kama yake

Read More