Baba Mtoto wa Sheebah Karungi Ajipata katika Tuhuma Nzito ya Wizi wa Magari Uingereza
Baba wa mtoto wa msanii nyota wa Uganda, Sheebah Karungi, amejikuta kwenye gumzo mitandaoni baada ya kuhusishwa na madai mapya ya uhalifu yaliyodaiwa kutokea nchini Uingereza. Kwa mujibu wa mwanablogu wa udaku Senga Acid, mume wa msanii huyo anayefahamika kama Jaffer aliwahi kuhukumiwa na kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka miwili kwa tukio la wizi wa magari nchini Uingereza. Inadaiwa kuwa taarifa hizo zilitolewa na aliyekuwa mkewe, Diana, ambaye alisemekana kupitia changamoto nyingi katika kipindi walichokaa pamoja. Senga amedai kuwa Diana ndiye aliyefichua tuhumu hiyo nzito dhidi ya Jaffer, ikiwemo madai ya kuhusika na kundi lililoripotiwa kuuza magari yaliyokuwa yakiibwa Uingereza na kusafirishwa Afrika Mashariki. Hata hivyo, hadi sasa hakuna nyaraka rasmi, rekodi za mahakama, wala taarifa za kuthibitisha madai hayo. Jaffer mwenyewe hajazungumza hadharani kuhusu tuhuma hizo, huku Sheebah na Diana pia hawajatoa kauli yoyote ya moja kwa moja kuhusiana na kilichoibuliwa. Tuhuma hizi zimeibuka wakati ambapo Sheebah Karungi anadaiwa kuvunja ndoa ya Diana kwa kuingia kwenye mahusiano na mume wake Jaffer ambaye amekuwa akivutia mashabiki na vyombo vya habari kufuatia habari za kuwa baba wa mtoto wa Sheebah.
Read More