SHILOLE ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE FACEBOOK

SHILOLE ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE FACEBOOK

Staa wa muziki wa bongofleva Shilole amesikitishwa na watu wanaotumia akaunti fake yenye jina lake katika mtandao wa Facebook kufanya uhalifu. Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole amesema hajawahi waitisha mashabiki zake pesa kupitia mtandao wa facebook ambapo amewataka mashabiki kuwa makini na matapeli wanaotumia jina lake kujipatia pesa kwani ukurasa wa facebook ambao walaghai wanatumia kuwaibia sio wake. Kauli ya Shilole inakuja mara baada ya kupokea lalama kutoka kwa mashabiki zake kuwa kuna akaunti ya Facebook inawatapeli pesa zao kupitia matangazo ya ajira yanayowekwa kwenye ukurasa feki unaotumia jina lake

Read More