Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Mtayarishaji wa maudhui mtandaoni, Shorn Arwa, amewakemea mastaa wanaodai kwamba wanachukia maisha ya umaarufu ilhali wao wenyewe huendelea kuchapisha maisha yao kwenye mitandao ya kijamii kila wakati. Kupitia instastory yake, Arwa amesema ni unafiki kwa mtu kulalamika kuhusu shinikizo la umaarufu lakini bado akawa wa kwanza kushiriki kila tukio la maisha yake hadharani. Mrembo huyo ameongeza kuwa mtu anayehisi kero na maisha ya umaarufu ana uwezo wa kuishi maisha ya kawaida bila kulazimika kutangaza kila hatua kwa mashabiki. Kauli ya Arwa imeibua maoni mseto miongoni mwa mashabiki na wanamitandao, baadhi wakikubaliana naye kwamba mastaa hawawezi kukwepa umaarufu endapo wao wenyewe ndio wanauendeleza. Wengine hata hivyo wameeleza kuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kuhisi kuchoshwa na presha za macho ya umma hata kama anapenda kushirikisha mashabiki wake.

Read More
 Shorn Arwa Awapa Somo Mabinti Baada ya Tukio la Aibu Luo Festival

Shorn Arwa Awapa Somo Mabinti Baada ya Tukio la Aibu Luo Festival

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuhusu maadili na kujithamini, akiwaasa kujitafutia fedha badala ya kutegemea wanaume kwa msaada wa kifedha. Kupitia mitandao ya kijamii, Arwa ameeleza masikitiko yake kufuatia matukio aliyoshuhudia katika tamasha la Luo Festival, akisema baadhi ya tabia zilizojitokeza ni za aibu na zinapaswa kukemewa. Arwa amedai kuwa baadhi ya warembo walijidhalilisha kwa kufanya vitendo vya aibu hadharani ili kupata tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo. Ameeleza kuwa wanawake wengi walijikuta wakifanya mapenzi na wanaume kwenye nyasi ili kupata tiketi, hali ambayo ametaja kuwa ya kusikitisha. Mrembo huyo amesisitiza kuwa kila mwanamke ana haki na uwezo wa kufanikisha maisha yake bila kulazimika kupitia njia za kudhalilisha utu wake. Pia amehimiza umuhimu wa wanawake kujitafutia kipato na kuepuka utegemezi wa kupita kiasi kwa wanaume, akiongeza kuwa mustakabali wa wanawake ni wenye matumaini makubwa. Ujumbe huo wa Shorn Arwa umeibua mjadala mitandaoni, wengi wakimuunga mkono kwa kuhimiza wanawake kujitegemea na kulinda heshima zao, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa elimu ya kujikimu kimaisha kwa vijana.

Read More