SIMI AFIKISHA STREAM MILLIONI MOJA BOOMPLAY

SIMI AFIKISHA STREAM MILLIONI MOJA BOOMPLAY

Mwimbaji nyota wa muziki toka nchini Nigeria, simi ambaye bado anaendelea kufanya vizuri na album yake mpya na ya tano iitwayo “To Be Honest” yenye mwezi mmoja tangu itoke, amejiunga rasmi na Golden Club ya Boomplay. Hatua hiyo kubwa kwa Simi inakuja baada ya streams zake zote za Boomplay kufika Milioni 100+ (100,000,000). Simi anakuwa msanii wa kwanza mwanamke kugonga streams hizo. Aidha, simi anajiunga na wasanii wengine wanaotesa katika anga la muziki kutoka Nigeria, ambao pia tayari wamefikisha idadi ya streams Milioni 100+ katika Boomplay, kama vile Davido, Wizkid, Burna Boy, Fireboy DML, Omah Lay, na Joeboy.

Read More
 SIMI AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

SIMI AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwimbaji nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Simi, ameachia rasmi album yake mpya iitwayo “To Be Honest”. Album hiyo ina jumla ya mikwaju 10 ya moto huku ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Adekunle Gold, Fave na Deja. To Be Honest ina nyimbo kama Story Story, No Joy, Balance, Born Again na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani. Hii inakuwa album ya tano kutoka kwa mtu mzima Simi baada ya “Restless II” iliyotoka mwaka 2020. Album zake nyingine ni pamoja na “Chemistry” (2016), “Simisola” (2017) na “Omo Charlie Champagne” (2019).

Read More
 SIMI MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

SIMI MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Msanii nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Simi, ametangaza kuachia album yake mpya mwezi ujao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Simi amethibitisha hilo akitoa maelezo kuwa album yake hiyo itaingia sokoni Juni 3 mwaka huu wa 2022. “Kiukweli kabisa album itatoka tarehe 3 mwezi wa 6”. Ameandika kwenye Instagram yake. Hii inaenda kuwa album ya tano kwa Simi  baada ya album yake ya “Restless II” iliyotoka mwaka 2020. Album zake nyingine ni pamoja na “Chemistry” ya mwaka wa 2016, “Simisola” ya mwaka wa 2017 na “Omo Charlie Champagne” ya mwaka wa 2019.

Read More
 SIMI AWEKA REKODI KWENYE MTANDAO WA AUDIOMACK AFRIKA

SIMI AWEKA REKODI KWENYE MTANDAO WA AUDIOMACK AFRIKA

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria, msanii Simi anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni ya nyimbo zake. Simi amefanikiwa kushika rekodi ya kuwa msanii wa kike Afrika kufikisha Streams Milioni 100 kwenye platform ya kuuzia muziki ya Audiomack kwa nyimbo zake zote. Hadi sasa ana jumla ya streams Milioni 124. Simi ambaye jina lake halisi ni Simisola Bolatito Kosoko kwa upande wa wasanii wa kike amewapiku wakali kama Tiwa Savage ambaye ana streams million 83.7M, Tems million 64.2, Yemi Alade million 24 na wengine wengi.

Read More