Nadia Mukami Atoa Kauli Nzito Kuhusu Single Mothers
Staa wa muziki, Nadia Mukami, amefunguka ya moyoni kuhusu unyanyapaa unaowakumba kina mama wanaolea watoto wao pekee yao (single mothers). Kupitia mitandao ya kijamii, Nadia ameeleza masikitiko yake kuhusu namna jamii imezoea kuwaelekezea lawama wanawake hao, huku ikiwapuuza kabisa wanaume waliokimbia majukumu yao ya malezi (deadbeat dads). Amebainisha kuwa sababu za mwanamke kuwa mama mlezi mmoja ni nyingi na halali, zikiwemo unyanyasaji wa majumbani, vifo vya waume, talaka, kutelekezwa, pamoja na uraibu wa dawa za kulevya au pombe kwa wenza wao. Ingawa amekiri kuwa si wanawake wote ni wakamilifu na baadhi huonyesha tabia zisizofaa katika co-parenting, Nadia amesisitiza kuwa lawama hazifai kuelekezwa kwa mwanamke pekee. Ametoa wito kwa jamii kujikita katika kutafuta suluhisho badala ya kuhukumu upande mmoja tu. Ujumbe wake huo umetambuliwa na wengi kama sauti ya matumaini kwa mamia ya kina mama wanaopitia hali hiyo kimya kimya. Mashabiki na wafuasi wake wamesifu msimamo wake wa kuthubutu kulizungumzia suala hilo kwa uwazi na kwa mtazamo wa huruma. Katika kuendeleza ujumbe huo, Nadia anatarajiwa hivi leo kuachia wimbo wake mpya “Single Mother”, ambao umetajwa kuwa sehemu ya harakati zake za kuangazia maisha na changamoto za mama mlezi mmoja kupitia muziki.
Read More