Leila Kayondo na mpenzi wake wa zamani SK mbuga wafufua tena penzi lao

Leila Kayondo na mpenzi wake wa zamani SK mbuga wafufua tena penzi lao

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Leila Kayondo amethibitisha kumaliza tofauti zake na mpenzi wake wa zamani SK mbuga baada ya wawili hao kutupiana maneno makali mtandaoni. Kupitia mahojiano yake Kayondo amesema kwa sasa yeye na SK Mbuga ni marafiki wakubwa huku akidai kuwa huwa wanazungumza mara kwa mara kuhusu masuala ya kibiashara na maisha kwa ujumla. Mrembo huyo amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayevunja urafiki wao kamwe, kitendo ambacho walimwengu wamehoji kuwa huenda amefufua tena penzi lake kwa bwenyenye huyo mwenye skendo nyingi za kutoka kimapenzi na wanawake tofauti. Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Leila Kayondo alikuwa gumzo nchini Uganda baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akitema nyongo kwa SK Mbuga kuwa asiwahi kayaga nyumbani kwake ambapo alienda mbali zaidi na kutishia kuanika maovu aliyomfanyia kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka 2010 hadi 2015.

Read More