Snoop Dogg Ahoji Maudhui ya Filamu ya Watoto Baada ya Kutazama Lightyear

Snoop Dogg Ahoji Maudhui ya Filamu ya Watoto Baada ya Kutazama Lightyear

Rapa mkongwe wa Marekani, Snoop Dogg, amesema kuwa hana tena amani ya kwenda kuangalia filamu kwenye sinema baada ya kushuhudia mjukuu wake akimuuliza maswali magumu alipowaona wahusika wa mapenzi ya jinsia moja wakionyeshwa kwenye filamu ya Lightyear. Kwa mujibu wa Snoop, alishtushwa na mjukuu wake kuuliza maswali baada ya kuona wapenzi wa kike (lesbian couple) ndani ya filamu hiyo ya watoto. Tukio hilo, amesema, lilimfanya ahisi wasiwasi kuhusu maudhui yanayoonyeshwa kwa watoto kupitia filamu kubwa za kimataifa. Kauli yake imezua mjadala mkubwa mtandaoni, baadhi ya watu wakieleza kuwa wasanii na wazazi wana haki ya kuamua maudhui ya watoto wao, huku wengine wakimkosoa kwa mtazamo wake wakidai anapinga usawa wa jamii ya LGBTQ+. Filamu ya Lightyear, ambayo ni tawi la hadithi maarufu ya Toy Story, ilizua gumzo kubwa tangu ilipoachiliwa mwaka 2022, hasa kwa sababu ya kuonyesha uhusiano wa ndoa wa jinsia moja kwa mara ya kwanza kwenye sinema ya Disney-Pixar.

Read More
 SNOOP DOGG AMUONGEZEA MSHAHARA ANAYEMTENGENEZEA BANGI

SNOOP DOGG AMUONGEZEA MSHAHARA ANAYEMTENGENEZEA BANGI

Rapper Snoop Dogg amemuongeza mshahara mfanyikazi wake anayemtengenezea bangi  (Personal blunt roller) kutokana na mfumuko wa bei. Akizungumza kwenye mahojiano na The Howard Stern Show, Snoop Dogg amesema nyongeza hiyo ya mshahara imetoka $40,000 hadi $50,000 ambayo ni sawa na takriban shillingi millioni 5,850,000 za Kenya kwa mwaka. Rapa huyo mkongwe kutoka Marekani mwaka 2019 alitusanua kwamba ameajiri mtu maalum kwa ajili ya kazi ya kutengeneza bangi tu.

Read More
 SNOOP DOGG ADOKEZA MPANGO WA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER

SNOOP DOGG ADOKEZA MPANGO WA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER

Rappa mkongwe kutoka Marekani Snoop Dogg ameibuka na kutangaza anataka kuununua mtandao wa Twitter Hii ni baada ya Bilionea Elon Musk kutangaza kwamba dili lake la kuinunua Kampuni ya Twitter imesitishwa kwa muda kufuatia uwepo wa akaunti bandia Sasa jmbo limemuibua Snoop Dogg kupitia ukurasa wake wa Twitter na ku-tweet yuko tayari kukamilisha ununuzi wa mtandao huo kwa kuandika ujumbe unaosomeka “Huenda watu wawili wakanunua Twitter sasa,” huku akisindikiza na hashtag #WhenSnoopBuysTwitter Snoop Dogg ameyataja mambo kadhaa ambayo atayafanya kama mmliki mpya wa mtandao huo wenye mamilioni ya wafuasi duniani kote, akiutaja mpango wa kumpa kila mtumiaji wa mtandao huo alama ya bluu iliyothibitishwa (Verification blue checkmark). “Kila mtu anapata alama ya bluu. hata roboti zenye majina yenye herufi 10 ambazo zinakufuata DM’s na kutoa tu salamu” ameeleza Dogg. Rapa huyo mwenye umri wa miaka 50, hata hivyo bado haijafahamika kwa undani zaidi ikiwa anadhamira ya dhati ya kuinunua Twitter baada Bilionea Elon Musk kutangaza kusitisha kwa muda.

Read More
 SNOOP DOGG ATHIBITISHA KUMILIKI MASTER RECORDINGS YA ALBUM YA DR. DRE “CHRONIC”

SNOOP DOGG ATHIBITISHA KUMILIKI MASTER RECORDINGS YA ALBUM YA DR. DRE “CHRONIC”

Rapa kutoka nchini Marekani Snoop Dogg amethitibisha kwamba sasa anamiliki masters (nakala asili) ya album maarufu ya Dr. Dre “Chronic” ambayo ilitoka chini ya Death Row Records. Hii imekuja kufuatia hivi karibuni kuanika wazi kuwa ameinunua label hiyo kongwe ya muziki. Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali, dili la Snoop Dogg kuinunua Death Row Records halijawekwa wazi lakini inasemekana atakuwa na umiliki wa baadhi ya kazi zilizotoka chini ya label hiyo ikiwemo pia za marehemu Tupac Shakur.

Read More
 RAPPER SNOOP DOGG KUFUNGULIWA KESI YA KUMDHULUMU DEREVA WA UBER

RAPPER SNOOP DOGG KUFUNGULIWA KESI YA KUMDHULUMU DEREVA WA UBER

Mkongwe wa muziki wa Hiphop nchini Marekani Snoop Dogg ameingia tena kwenye Headline Baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Akimporomoshea Matusi Dereva wa Uber Eats kwa kushindwa kumpeleka chakula. Kwenye kipande cha video hiyo alichoshare kwenye Instagram page yake Snoop Dogg anaskika akimtusi Dereva huyo kwa hasira. “Chakula changu kiko wapi Umepata pesa zako zote Chakula kiko wapi.” Kulingana na ripoti ya Complex, Dereva alifika na hakuwa na uhakika ni wapi pa kupeleka chakula hicho, kwa kuwa Auncle Snoop hakuwa mahali salama, ikizingatiwa kuwa alizidi kumuelekeza asogee Kwenye Geti Nyeusi aache chakula alicho muagiza. Inaelezwa kuwa Dereva wa (Uber) Amemfungulia kesi Snoop Dogg kwa kumuhatarishia usalama wake kwa Kinachononekana kwenye video hiyo. Kwa Mujibu wa Chanzo kilichopo karibu na Dereva uber kimemnukuu Dereva akisema “Ni picha yangu Hapo pia kuna jina langu la kwanza,..” Baada ya kuona video, imenipa wasiwasi, mwingi na ninahofia usalama wa familia yangu. Niliwasiliana na mteja Mara nyingi na nikafuata itifaki ya Ramani..Ila hakuwa sehemu salama” .Dereva, aitwaye Sayd, alisema.

Read More
 SNOOP DOGG AFUNGULIWA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

SNOOP DOGG AFUNGULIWA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO

Mkongwe wa muziki wa HipHop kutoka nchini Marekani Snoop Dogg amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na mwanamke mmoja, kufuatia tukio ambalo lilitokea mwaka 2013. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Mei 29, mwaka wa 2013 mwanamke huyo ambaye hakutaja jina lake amesema alihudhuria moja ya onesho la Snoop Dogg mjini Anaheim, California. Snoop Dogg alikuwa na swahiba wake aitwaye Bishop Don Juan na walimpatia ‘lift’ mwanamke huyo ambaye hakuwa na usafiri usiku akiwaomba wamfikishe nyumbani kwake. Baada ya kupatwa na usingizi kwenye gari, mwanamke huyo amedai kwamba badala ya kupelekwa kwake, alijikuta asubuhi yupo nyumbani kwa Bishop Don Juan kitandani na alikuwa akitoa Uume wake na kumwekea usoni. Baadaye alimpa nguo ya kuvaa na kuelekea studio kwa Auncle Snoop. Baada ya kufika studio, mwanamke huyo anasema hali yake ilikuwa sio nzuri, hivyo akaomba aingie chooni, akiwa huko anasema alimuona Snoop Dogg akiingia na kusimama mbele yake akiwa ametoa uume wake nje na kumwekea usoni, kisha alianza kumlazimisha kufanya ngono ya mdomo yaani Oral Sex. Hata hivyo upande wa mtu mzima Snoop Dogg umejitokeza na kusema kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote na mwanamke huyo anajitafutia pesa tu.

Read More
 RAPPER SNOOP DOGG AINUNUA LEBO YA MUZIKI YA DEATH ROW RECORDS

RAPPER SNOOP DOGG AINUNUA LEBO YA MUZIKI YA DEATH ROW RECORDS

Ni rasmi sasa mkongwe wa Hiphop kutoka Marekani Snoop Dogg ndiye mmiliki wa lebo ya muziki ya Death Row Records. Rapa huyo amenunua haki zote za lebo hiyo kongwe ambayo ilimtambulisha kwenye muziki miaka 30 iliyopita. Death Row Records ilikuwa inamilikiwa na kampuni ya MNRK Music Group. Kwa mujibu wa taarifa kwa Waandishi wa habari ambayo imetolewa, Snoop Dogg ataiongoza Death Row Records kwa miaka ijayo akiwa kama mmiliki mpya. Auncle Snoop alijiunga na lebo hiyo mwaka wa 1993 ambapo aliachia album yake ya kwanza, Doggy Style. Death Row Records ilianzishwa na Dr. Dre, Suge Knight, The D.O.C. na Dick Griffey mwaka 1991 na imekuwa nyumba ya historia kwa kuwatoa wakali wa Hop Hop Marekani kutoka West Coast.

Read More
 RAPPER SNOOP DOGG KUJA NA BIDHAA ZENYE KUTUMIA NYAMA YA MBWA

RAPPER SNOOP DOGG KUJA NA BIDHAA ZENYE KUTUMIA NYAMA YA MBWA

Miaka sita baada ya kusema kuwa “kamwe hatokula tena nyama au bidhaa zenye nyama ya mbwa” rapper mkongwe kutoka, Marekani Snoop Dogg anapanga kuzindua chapa au bidhaa zake inayoitwa “Snoop Doggs,” zitakazo tumia nyama ya mbwa. Kulingana na uwasilishaji wa kisheria wa hivi majuzi mawakili wa nguli huyo wa hip-hop walituma maombi mwezi uliopita katika ofisi ya patent ya marekani ili kusajili jina hilo kibiashara. Mawakili wa rapa huyo wamesema snoop ametumia jina la “snoop doggs,” wakisema ana mpango wa kulitumia kuuza hot dogs na aina nyingine za sausage.

Read More
 50 CENTS ATANGAZA KUJA NA SERIES MPYA “QUEEN NZINGA”

50 CENTS ATANGAZA KUJA NA SERIES MPYA “QUEEN NZINGA”

Mkongwe wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani 50 Cent ameuweka muziki kando, anaendelea kujikita kwenye upande wa kutayarisha filamu na vipindi vya televisheni. Siku chache baada ya kutangaza kuja na series ‘Murder Was the Case’ ambayo itagusia historia ya kweli ya rapa Snoop Dogg, 50 Cent ametangaza tena ujio wa series mpya nyingine chini ya Starz. Kupitia ukurasa wake wa instagram, 50 Cent alitudokeza kuhusu ujio wa series iitwayo ‘Queen Nzinga’ ambayo itaangazia na kujikita kwenye maisha ya malkia huyo wa Kiafrika katika Karne 17 nchini Angola. Uhusika mkuu utavaliwa na Yetide Badaki ambaye pia ni mtayarishaji mkuu series hiyo.

Read More
 50 CENT KUILETA “MURDER WAS THE CASE” KWENYE RUNINGA YAKO AKISHIRIKIANA NA SNOOP DOGG

50 CENT KUILETA “MURDER WAS THE CASE” KWENYE RUNINGA YAKO AKISHIRIKIANA NA SNOOP DOGG

Mwaka 1993 wakati Snoop Dogg akirekodi album yake ‘Doggystyle’ alikumbana na kesi ya mauaji kufuatia Kifo cha member wa kundi hasimu ambapo ilidaiwa aliuawa kwa kupigwa risasi na bodyguard wa Snoop Dogg. Album hiyo ya Snoop Dogg ilienda sambamba na usikilizwaji wa kesi yake kiasi cha kupelekea mauzo ya album hiyo kupaa juu na kutengeneza historia kufuatia pia wimbo ‘Murder Was the Case’ uliokuwemo kwenye album hiyo. 50 Cent akiwa kama mtayarishaji mkuu ametangaza ujio wa series iitwayo ‘Murder Was the Case’ chini ya STARZ akishirikiana na rapa Snoop Dogg ambapo itaangazia kisa chote cha tukio hilo ambalo lilimuweka Snoop chini ya ulinzi hadi February 20, 1996 alipoachiwa huru.

Read More
 SNOOP DOGG AINGIZA MABILLIONI YA FEDHA KUPITIA KAMPUNI YA BANGI

SNOOP DOGG AINGIZA MABILLIONI YA FEDHA KUPITIA KAMPUNI YA BANGI

Licha ya kuwa mtumiaji maarufu, Snoop Dogg ni mwekezaji kwenye biashara ya bangi. Kwa mujibu wa Bloomberg, kampuni ya Dutchie ambayo Snoop amewekeza pesa zake tangu mwaka 2018 imepanda thamani na kufikia takriban shillingi billioni 388. Kampuni hiyo iliyopo Oregon nchini Marekani ilianza kufanya vizuri kifedha miezi saba iliyopita kwa kutajwa kuwa na thamani ya shillingi billioni 188 na imeendelea kukua siku hadi siku tangu kuhalalishwa kwa zao la bangi kwenye maeneo mengi nchini Marekani. Ikumbukwe, mapema mwaka huu kampuni nyingine ya “Cannabinoid Technologies” ambayo Uncle Snoop amewekeza ilipanda thamani na kufikia shillingi billioni 7.5. Snoop pia ana bidhaa zake za bangi ziitwazo Leafs By Snoop.

Read More