Klabu ya Fiorentina haina  mpango wa kumuuza mchezaji wa Morocco Sofyan Amrabat

Klabu ya Fiorentina haina mpango wa kumuuza mchezaji wa Morocco Sofyan Amrabat

Mkurugenzi wa klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A ameeleza hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Morocco Sofyan Amrabat mwenye umri wa miaka 26. Kiungo huyo ambaye ameonesha ubora mkubwa kwenye michuano ya kombe la dunia huku akiisaidia timu yake ya taifa ya Morocco kufika hatua ya Nusu Fainali kwa kufanya vyema mbele ya vigogo kama Ubelgiji, Croatia, Spain na Ureno, Mkurugenzi wa Fiorentina alipoulizwa kuhusu kiungo huyo kusepa Januari alikanusha taarifa hiyo. “Hatuna mpango wa kumuuza. Tuna nafasi ya kumuongezea mkataba, Hatuna haja ya kuharakisha kwasababu yupo kwenye mipango yetu.” ameeleza Sofyan Amrabat kwa sasa amekua akihusishwa na vilabu vikubwa na hiyo ni kutokana na ubora mkubwa aliouonesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Read More