Sosuun Atoa Somo kwa Mabinti Kuhusu Maisha Bila Watoto
Msanii maarufu wa Kenya, Sosuun, ameibua mjadala mkubwa baada ya kutoa ujumbe mzito unaolenga mabinti nchini kuhusu uamuzi wa kutokuwa na watoto. Kupitia video yake Instagram, Sosuun alisema kuwa kutokuwa na watoto kunaweza kuonekana kama uamuzi sahihi katika kizazi cha sasa, hasa kwa kuzingatia changamoto za mahusiano yasiyodumu na watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili. Hata hivyo, aliwaonya mabinti kutofanya maamuzi hayo kwa misingi ya mitindo inayotrend mitandaoni bila kujitafakari kwa undani. Sosuun alisisitiza kuwa maisha ya uzee huja na changamoto zake, ikiwemo kupoteza nguvu, maradhi, na kuhitaji msaada wa kihisia na kimwili. Katika wakati kama huo, familia na watoto mara nyingi huwa nguzo muhimu ya msaada. “Fikiria kwa kina kabla ya kuamua, usifanye kwa sababu kila mtu anafanya,” alisema Sosuun. Ujumbe huo umetajwa kama somo kwa mabinti nchini Kenya, wengi wakimpongeza msanii huyo kwa kuzungumza ukweli unaoangazia thamani ya familia na malezi, huku mjadala ukiendelea mitandaoni kuhusu uhuru wa maamuzi ya kibinafsi.
Read More