TikTok na SoundCloud Waanzisha Ushirikiano Mpya wa Kusaidia Wasanii na Wapenzi wa Muziki

TikTok na SoundCloud Waanzisha Ushirikiano Mpya wa Kusaidia Wasanii na Wapenzi wa Muziki

TikTok imeingia kwenye ushirikiano rasmi na SoundCloud, hatua inayolenga kuimarisha uzoefu wa watumiaji wa majukwaa hayo mawili na kusaidia wasanii wanaoibukia. Kupitia makubaliano hayo mapya, nyimbo kutoka SoundCloud sasa zitapatikana moja kwa moja kwenye TikTok, huku watumiaji wakipewa uwezo wa kuzihifadhi kupitia kipengele kipya kiitwacho “Add to Music” kwenye maktaba yao ya muziki (Library). Hili ni jukwaa jipya la fursa kwa wasanii walioko SoundCloud ambao bado hawajaanza kuweka nyimbo zao kwenye majukwaa makuu ya kimataifa kama Spotify, Deezer na Apple Music. Kupitia mfumo huu, watapata mwangaza mpana zaidi kupitia video za TikTok ambazo mara nyingi huwa zinachochea mafanikio ya nyimbo mitandaoni. TikTok tayari ina ushirikiano sawa na Spotify na Apple Music, lakini ujio wa SoundCloud kwenye mkataba huu unaongeza kina na utofauti wa orodha ya muziki kwenye mtandao huo maarufu wa video fupi. Wataalamu wa muziki wanasema mabadiliko haya yanaweza kubadilisha kabisa taswira ya jinsi muziki unavyogunduliwa na kusambazwa kwa mashabiki wapya duniani.

Read More