Rayvanny Kutumbuiza Uwanja wa Taifa Juba, South Sudan
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, anatarajia kutikisa jiji la Juba, South Sudan kwa onyesho kubwa litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Juba (Juba National Stadium). Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Rayvanny amethibitisha taarifa hiyo kwa maneno mazito yaliyojaa kujiamini, akieleza kuwa yeye si msanii wa kumbi ndogo bali wa viwanja vikubwa. “Not Arena, we do stadiums! #JUBANATIONALSTADIUM I #GLOBALWAY!!! #SouthSudan NIAMINI MIMI HAPA PATAKUA HAKUNA PA KUKANYAGA,” ameandika Rayvanny. Kauli hiyo imezua gumzo kubwa mitandaoni, huku mashabiki wake wakionyesha shauku ya kumuona akiangusha burudani ya nguvu mbele ya maelfu ya mashabiki wa South Sudan. Onyesho hilo linaelezwa kuwa sehemu ya safari yake ya kimataifa ya muziki, inayolenga kufikisha sauti ya Bongo Fleva mbali zaidi kimataifa. Rayvanny, ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Next Level Music, anaendelea kudhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaopiga hatua kubwa katika anga za kimataifa.
Read More