Wasanii Waathirika na Marufuku ya Betting, Ssaru Asema Wameachwa Bila Kipato

Wasanii Waathirika na Marufuku ya Betting, Ssaru Asema Wameachwa Bila Kipato

Mwanamuziki wa gengetone Sylvia Ssaru, maarufu kama Ssaru, amefunguka kwa uchungu kuhusu athari za marufuku ya Bodi ya Kudhibiti Kamari nchini Kenya (BCLB) dhidi ya matangazo ya betting kupitia influencers na wasanii. Akizungumza na SPM Buzz katika mahojiano maalum, Ssaru alisema marufuku hiyo imeathiri moja kwa moja kipato chake na cha wasanii wengine waliokuwa wakitegemea mikataba ya ubalozi kutoka kwa kampuni za kubashiri. “Ni kama tumetolewa nyama kwa mdomo. Hapa ndo tunatoanga rent, pesa za video. Kuna influencer labda hii ndo deal yake ya kwanza, na sasa they consider themselves jobless,” alisema. Kauli ya Ssaru imekuja siku chache tu baada ya BCLB kutoa agizo rasmi likipiga marufuku kampuni za kubashiri kutumia influencers, wanablogu, na majukwaa ya mitandao ya kijamii kama sehemu ya mikakati yao ya matangazo. Katika waraka uliotumwa kwa kampuni mbalimbali, BCLB ilisema kuwa matumizi ya watu maarufu katika kuchochea tabia ya kubashiri ni kinyume na sheria na inahatarisha kizazi cha sasa, hasa vijana. Hii imeacha pengo kubwa kwa wasanii na maudhui wa dijitali ambao walikuwa wakitegemea kampeni hizo kama chanzo mbadala cha mapato katika tasnia isiyo na uhakika wa kipato wa kila siku.

Read More
 Rapa Sylivia Ssaru atangaza kuja na Album mpya mwaka 2023

Rapa Sylivia Ssaru atangaza kuja na Album mpya mwaka 2023

Rapa wa kike nchini Ssaru ameweka wazi kuna huenda akaachia album ama EP mwanzo mwa mwaka 2023. Kwenye mahojiano na Plug TV Ssaru amesema anaendelea na mchakato wa kuitayarisha mradi wake mpya ambao kwa mujibu wake amewashirikisha wasanii wa ndani na nje ya Kenya. Mrembo ambaye mapema mwaka huu aliahidi kuachia EP mpya amewataka mashabiki kuwa na subira kipindi hiki yupo kwenye matayarisho ya mwisho ya kukamilisha kazi yake. Lakini amenyosha maelezo kuhusu uhusiano wake na msanii Trio Mio kutokana na watu kumhusisha kutoka nae kimapenzi kwa kusema kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii huyo ambapo amedai ukaribu wao ni wa kikazi kama namna akifanya na wasanii wa kiume. Hata hivyo amewataka watu kukoma kumhusisha kimapenzi na Trio Mio na badala yake wategemea makubwa kutoka kwao ikizingatiwa wana uhusiano mzuri kisanaa.

Read More
 SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

Female rapper kutoka Kenya Sylvia Ssaru ameibuka na kukanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na msanii mwenzake Trio Mio. Hii ni baada ya wawili hao kuonekana kuwa na ukaribu katika siku za hivi karibuni toka walipoachia ngoma ya pamoja iitwao “Kichwa tu” ambayo wamemshirikisha Timmy Tdat. Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka kujua kama kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Trio Mio kwenye mtandao wa instagram Ssaru amesema hakuna kitu chochote kinaendelea kati yake na trio mio huku akidai kuwa uhusiano wao utabaki kuwa wa ndugu na dada. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumshambulia Ssaru ambapo wengi wamedai kuwa mrembo huyo ambaye ni mkubwa kiumri ana mpango wa kumharibu kimaadili Trio Mio ambaye bado anasoma shule ya upili.

Read More