Video Mpya Yazima Uvumi: Cardi B na Stefon Diggs Wapo Bado Kwenye Mahaba

Video Mpya Yazima Uvumi: Cardi B na Stefon Diggs Wapo Bado Kwenye Mahaba

Tetesi kuwa uhusiano kati ya rapa maarufu Cardi B na mcheza mpira wa Marekani Stefon Diggs umeenea mitandaoni, lakini taarifa mpya zinaonyesha kuwa penzi lao bado lipo imara. Uvumi wa kuachana kwao ulianza baada ya mashabiki kubaini kuwa Cardi B alikuwa amefuta picha zote za Stefon Diggs kwenye akaunti yake ya Instagram, jambo lililoibua maswali mengi kuhusu mustakabali wa uhusiano wao. Hata hivyo, Cardi B alionekana kupuuzilia mbali uvumi huo kwa kuchapisha video kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), akionekana akiwa gym na Diggs wakifanya mazoezi pamoja. Video hiyo imechukuliwa kama jibu kwa waliodhani kuwa wawili hao tayari wameachana. Chanzo cha karibu na wawili hao kimeripotiwa kuiambia TMZ kwamba wapenzi hao bado wako kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaendelea vyema, tofauti na taarifa zinazozunguka mtandaoni.

Read More
 Cardi B Aibua Sintofahamu Baada ya Kufuta Picha za Stefon Diggs

Cardi B Aibua Sintofahamu Baada ya Kufuta Picha za Stefon Diggs

Mashabiki wa rapa maarufu Cardi B wameibua hisia mseto mitandaoni baada ya kugundua kuwa msanii huyo amefuta picha zote za mpenzi wake mpya, Stefon Diggs, kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hatua hiyo imezua tetesi kuwa huenda uhusiano wao umeingia matatizoni au hata kuvunjika kabisa. Wengi wa mashabiki walieleza mshangao na masikitiko, wakikumbuka jinsi penzi la Cardi na Stefon lilivyokuwa linaonekana kuwa la kipekee, lenye mapenzi ya dhati na hadhi ya juu. Wengine walitafsiri hatua hiyo kama njia ya Cardi kujilinda dhidi ya maisha ya umma, huku baadhi wakiamini ni dalili ya mgogoro wa kimapenzi unaoendelea kisiri. Penzi kati ya Cardi B na Stefon Diggs lilianza rasmi mwezi Juni 2025, walipoonekana kwa mara ya kwanza hadharani wakiwa kwenye boti ya kifahari, wakifurahia muda wao pamoja. Baadaye walihudhuria kwa pamoja Paris Fashion Week na mechi ya mpira wa vikapu jijini New York kati ya Knicks na Celtics, hali iliyothibitisha wazi kuwa walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. Katika tamasha la Cannes, Cardi alionyesha upendo wake kwa Stefon kwa kuchora jina lake kwenye kucha zake, jambo lililozua gumzo mitandaoni. Mwisho wa mwezi Juni, wawili hao walikwenda mapumzikoni nchini Ufaransa ambapo Stefon alimkodishia Cardi kasri la kifahari kwa ajili ya likizo ya faragha. Hata hivyo, kufutwa kwa picha hizo kumezua hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wa uhusiano huo, hasa ikizingatiwa kuwa Cardi bado yuko katika mchakato wa talaka kutoka kwa mume wake wa zamani, Offset. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka kwa mmoja wao ili kufahamu hatima ya penzi hili lililoanza kwa kishindo.

Read More
 Cardi B afunguka kuhusu msimamo wa mpenzi wake Stefon Diggs licha ya misukosuko

Cardi B afunguka kuhusu msimamo wa mpenzi wake Stefon Diggs licha ya misukosuko

Rapa maarufu Cardi B amefichua kuwa mchezaji wa NFL, Stefon Diggs, alimshauri aache kushiriki mambo ya faragha hadharani. Katika mahojiano ya hivi karibuni, Cardi alisema kuwa Diggs alipendekeza awe na mipaka kwenye kile anachoweka mitandaoni au anachosema hadharani kuhusu maisha yao binafsi. Cardi B pia alieleza kuwa licha ya mahusiano yao, wawili hao huonana mara mbili tu kwa wiki kutokana na ratiba zao kuwa na shughuli nyingi. Hata hivyo, uhusiano wao umekumbwa na changamoto.  Hivi karibuni, video ilisambaa ikimuonyesha Diggs akiwa kwenye boti na wanawake wengine, jambo lililomfanya Cardi B kueleza hisia zake za kukerwa na tabia hiyo. Licha ya matatizo hayo, wawili hao walionekana pamoja hadharani kwa mara ya kwanza wakiwa wameshikana mikono katika mchezo wa NBA kati ya Boston Celtics na New York Knicks kwenye uwanja wa Madison Square Garden mnamo Mei 12, 2025. Kwa sasa, mashabiki wanaendelea kufuatilia maendeleo ya uhusiano wao, wakijiuliza ikiwa wataweza kushinda changamoto zilizopo na kuendeleza penzi lao.

Read More