BASATA YASITISHA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

BASATA YASITISHA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

Baraza la Sanaa la Tanzania – BASATA limemtaka Msemaji wa Shirikisho la Muziki nchini humo, Steve Nyerere asianze kutekeleza majukumu yake hadi pale mamlaka hiyo itakapofahamu kiini cha mgogoro wa uteuzi wake na kupata ufumbuzi kwa mujibu wa katiba na sheria. BASATA imesema inafanyia kazi taarifa zilizowasilishwa na shirikisho pamoja na hoja za wajumbe waliohudhuria kikao kilichofanyika machi 21 mwaka huu kuhusu uteuzi wa nafasi hiyo, ambapo katika kikao hicho wadau wa muziki tanzania walisema Steven Nyerere hawezi kuwa msemaji wala mhamasishaji wa muziki.. Hata hivyo Muda mfupi baada ys Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumtaka Steve Nyerere kutoanza kazi kama Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania, msanii huyo ameshukuru kwa kusema kwamba anaheshimu uamuzi huo. “Niseme asante Basata, asante sana haki inabaki pale pale, pole jirani na tupo pamoja yaliyopita si ndwele tugange yajayo” “Basata imesema kwamba sasa inafanyia kazi taarifa ya shirikisho na hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao.” ameandika Steve Nyerere Instagram.

Read More
 STEVE NYERERE: SITOJIUZULU KAMA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

STEVE NYERERE: SITOJIUZULU KAMA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania Steve Nyerere amedai kwamba hatojiuzulu kwenye wadhfa wake licha ya shinikizo anazozipokea kutoka kwa baadhi ya wasanii. Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Nyerere amesema uteuzi wake ukitenguliwa atakata rufaa mahakamani huku akisisitiza kuwa ana nia njema ya kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Bongofleva. “Sijiuzulu na wala sitoki, nina nia ya kuendeleza industry ya nchi hii.” Amesema Steve Nyerere Ikumbukwe juzi kati wakati kamati la Shirikisho la muziki Tanzania lilimteua Steve Nyerere kuwa msemaji wa shirikisho hilo, wadau wengi wa sanaa nchini Tanzania walipinga vikali uteuzi wake wakidai kuwa hana vigezo kabisa vya kuwasimamia wanamuziki. Hata hivyo Mwenyekiti wa shirikisho la wasanii Tanzania Rapa Fid Q alipokea maoni ya waliopinga uteuzi wa Steve Nyerere kwa mikono miwili ambapo alienda mbali zaidi na kutangaza mkutano utakaowaleta pamoja wadau mbali mbali wa sanaa, Machi 21, 2022 kujadili mustakabali wa shirikisho hilo.

Read More