STEVO THE SIMPLE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

STEVO THE SIMPLE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

Msanii Stevo the Simple Boy hataki kupoa kabisa kwenye suala la kuupeleka muziki wake kimataifa, hii ni baada ya kutangaza ujio wa tamasha lake la muziki. Kupitia ukurasa wake wa Iinstagram Stevo amesema tamasha lake litaitwa freshi barida huku akiwaachia mashabiki swali kama watanunua tiketi za tamasha hilo ambalo anajianda kuja na nayo hivi karibuni. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ni Nani” amesema anaenda kuweka historian nchini na afrika kwa ujumla kupitia freshi barida concert huku akiwataka mashabiki zake wapendekeze wasanii wao pendwa ambao wangependa awajumuishe kwenye tamasha lake hilo. “TULIONA SHINCITY NASASA TUTAONA FRESHI BARIDA CONCERT… HISTORIA ITAONEKANA NCHINI KENYA NA AFRICA MZIMA… JE UTANUNUA TIKITI? NA UNATAKA KUWAONA WASANI WAGANI KWENYE CONCERT YANGU?”, Ameandika kupitia Instagram yake.. Kauli ya Stevo imekuja mara baada ya kuachia wimbo wake mpya uitwao freshi barida siku kadhaa baada ya kutasanua kuwa anakuja na kinywaji chake kiitwacho freshi barida energy.

Read More
 STEVO THE SIMPLE BOY MBIONI KUZINDUA ENERGY DRINK YAKE

STEVO THE SIMPLE BOY MBIONI KUZINDUA ENERGY DRINK YAKE

Inaonekana Msanii Stevo The Simple anataka kugeuza muziki wake kuwa biashara mara baada ya kutangaza  ujio wa kinywaji chake kiitwacho ”Freshi Barida” Msanii huyo amethibitisha taarifa hiyo njema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kwa kuachia mashabiki zake swali kama watauunga mkono atakapoingiza bidhaa hizo sokoni. Stevo the Simple ni moja ya wasanii chipukizi katika tasnia ya muziki nchini Kenya jitihada zake na uwezo wake umekuwa ukionekana kupitia kazi mbalimbali anazozifanya, kama msanii anayechipukia, hii ni moja ya hatua kubwa katika muziki. Utakumbuka Stevo ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Men in business amekuwa akitangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni Aprili 28 mwaka huu.

Read More