Stivo Simple Boy akiri kuchumbiwa na wanawake wenye umri mkubwa

Stivo Simple Boy akiri kuchumbiwa na wanawake wenye umri mkubwa

Msanii Stivo Simple Boy amefunguka usiyoyajua kuhusu maisha yake kwa kusema kuwa wanawake wenye umri mkubwa wamekuwa wakimzimia kimapenzi kupitia mitandao ya kijamii. Kwenye mahojiano na Mwende Macharia msanii huyo wa Men in Business amesema wanawake hao wamekuwa wakimuahidi maisha mazuri huku wakimsisitizia kwamba hawatokuja kumkimbia ikitokea ameridhia ombi la kuingia nao kwenye mahusiono. Hitmaker huyo “Freshi Barida” amesema kwamba hayuko tayari kutoka kimapenzi na wanawake waliomzidi umri kwa sababu watamkimbia akifilisika kiuchumi. “Wana pesa ndio maana wanadhani nitakubali kutoka nao kimapenzi. Sitaki kujihusisha nao kwa sababu watanikimbia nikifilisika.”, Alisema. Simple Boy hajakuwa kwenye mahusiano yeyote ya kimapenzi tangu alipoachana na mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy kwa madai ya usaliti.

Read More
 PRITTY VISHY AFUNGUKA SABABU ZA KUTOHUDHURIA HARUSI YA STIVO SIMPLE BOY

PRITTY VISHY AFUNGUKA SABABU ZA KUTOHUDHURIA HARUSI YA STIVO SIMPLE BOY

Ex wa msanii Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni baada ya kukiri hadharani kuwa atahudhuria harusi ya mkali huyo wa ngoma ya Freshi Barida. Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram vishy amesema anaogopa makalio yake yaatamchanganya kimawazo Stivo kwenye siku yake hiyo muhimu. Sanjari na hilo amesema haoni ndoa ya Stivo na mpenzi wake Gee ikidumu kwa kuwa anajua uyonge wa msanii huyo linapokuja suala la unyumba. Hata hivyo amemtolea uvivu msanii huyo wa Men in Business kutokana na suti aliyokuwa amevaa juzi kati kwa kusema kwamba mtindo wa suti hiyo ni wa kizamani sana, hivyo waliomvalisha walifeli kinoma. Utakumbuka Vishy ambaye anaidaiwa kutoka kimapenzi na msanii Madini Classic alikuwa kwenye mahusiano na Stivo Simple Boy lakini walikuja wakaachana kutokana na madai ya usaliti.

Read More
 MENEJA VAGA AMKINGIA KIFUA STIVO SIMPLE BOY KWA TUHUMA ZA WIZI

MENEJA VAGA AMKINGIA KIFUA STIVO SIMPLE BOY KWA TUHUMA ZA WIZI

Meneja wa Stivo Simple Boy Vaga amevunja kimya chake kuhusu tuhuma zilizotembea mtandaoni kuwa msanii wake alimuiba mpenzi wa mtu. Katika mahojiano yake na Captain Nyota vaga amesema madai ya Stivo kumchukua mpenzi wa mtu hayana ukweli wowote bali yanatumiwa na baadhi ya watu mtandaoni  kama daraja la kupata umaarufu kwenye vyombo vya habari nchini. Aidha amesema Stivo alimpata mpenzi wake kwa njia ya halali huku akisema msaniii huyo yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake ikiwa ni siku chache zimepita tangu wavishane pete ya uchumba. Kauli ya Vaga imekuja mara baada ya wanaume wawili kujitokeza kwenye nyakati tofauti na kudai kuwa stivo aliwaibia mpenzi wao kitu ambacho ambacho stivo mwenyewe alikanusha vikali mapema wiki hii.

Read More
 STIVO SIMPLE MBIONI KUJA NA FRESHI BARIDA ENERGY DRINK

STIVO SIMPLE MBIONI KUJA NA FRESHI BARIDA ENERGY DRINK

Msanii Stivo Simple Boy amedokeza mpango wa kuja na kinywaji chake laini (soft drinks) kiitwacho Freshi Barida. Kupitia ukurasa hitmaker huyo wa Glory amesema kinywaji chake hicho itaingia sokoni au itapatikana kwenye maduka yote nchini hivi karibuni kama mipango yake itaenda vizuri. “ Na mungu akituzidia zitakua madukani Ivi karibuni tukue freshi barida’” Ameandika Instagram Utakumbuka Stevo, pamoja na uongozi wake mapema mwaka huu walizindua chapa ya mavazi iitwayo Freshi Barida na tangu ujio wake imepokelewa kwa ukubwa na mashabiki  ambao wamekuwa wamekuwa wakimsapoti Stivo kwa kununua mavazi hayo. Neno Freshi Barida imekuwa maarufu miomgoni mwa wakenya  na ni jina ya wimbo wa msanii huyo ambao unazidi kufanya vizuri youtube ikiwa na Zaidi ya watazamaji laki 8 huku remix yake ikiwa na watazamaji laki 4.5 ndani ya wiki moja.

Read More
 STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA KUTUPWA JELA KISA TUHUMA ZA UBAKAJI

STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA KUTUPWA JELA KISA TUHUMA ZA UBAKAJI

Msaniii Stivo Simple Boy ametupasha tusiyoyajua kuhusu maisha yake. Katika mahojiano na Obinna tv Stivo amesema kuna kipindi alitupwa jela kwa wiki moja baada ya mrembo mmoja kumsingizia tuhuma za ubakaji. Hitmaker huyo wa ‘Freshi Barida” amesema purukushani kati yake na mrembo ilianza kipindi alipomkata kimapenzi jambo lilimfanya akamshataki kwa mama yake mzazi kuwa alimbaka na hapo ndipo akajipata jela. Hata hivyo amesema kesi yao ilipokuwa ikiendelea alipelekwa na mrembo huyo hospitali ambapo walifanyiwa vipimo lakini walipotoa matokea ilibainika kwamba madai ya kumbaka mrembo huyo hayakuwa na ukweli wowote, hivyo akaachiwa huru.

Read More
 STIVO SIMPLE BOY ATANGAZA KUACHIA REMIX YA FRESHI BARIDA

STIVO SIMPLE BOY ATANGAZA KUACHIA REMIX YA FRESHI BARIDA

Msanii wa lebo ya muziki ya  Men in Business Stivo Simple Boy ameweka wazi kuachia remix ya smash hit yake iitwayo “Freshi Barida”. Wimbo ambao bado unaendelea kufanya vizuri kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni. Stivo Simple Boy ametangaza uwepo wa remix hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amedokeza mpango wa kumshirikisha Mejja, Exray na mkali wa muziki wa Amapiano Ntoshi Gazi kutoka Afrika Kusini kwenye remix ya wimbo wa Freshi Barida. Kulingana na Meneja wa Stivo aitwaye Vaga, wimbo huo utaingia sokoni juma lijalo na tayari mchakato wa kutayarisha video umeanza huku wasanii walioshirikishwa wakitarajiwa kuhusika kikamilifu kwenye maandalizi ya project hiyo. Video ya Wimbo wa Freshi Barida ina zaidi ya views laki saba kwenye mtandao wa youtube tangu iachiwe rasmi mwezi mmoja uliopita.

Read More
 CARTOON 47 ALALAMIKA KUTENGWA KWENYE MAFANIKIO YA WIMBO WAKE MPYA

CARTOON 47 ALALAMIKA KUTENGWA KWENYE MAFANIKIO YA WIMBO WAKE MPYA

Msanii Cartoon 47 ameonesha kutoridhishwa na mapokezi ya wimbo wake mpya uitwao Haiwezi ambao amemshirikisha Stevo Simple Boy na Ntosh Ngazi. Katika mahojiano yake hivi karibuni Cartoon 47 amesema watu wamekuwa wakimchukulia stevo kama mmiliki wa wimbo huo wakati yeye ndiye aligharamia mchakato wa kutayarisha wimbo wenyewe kwa kumleta Ntosh Gazi kutoka Afrika Kusini. Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba jambo hilo limepelekea baadhi ya mapromota kuanza kumpendelea Stevo  kwenye shoo zao huku wakimtenga. Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wa muziki nchini kutomchukulia poa kwenye muziki wake na badala yake watambua pia mchango wake kwenye mafanikio ya wimbo huo. Wimbo huo uitwao Haiwezi wenye mahadhi ya Amapiano unafanya vizuri kwenye majukwaa mbali mbali ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni ambapo kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views laki 1 ndani siku 5 tangu iachiwe rasmi.

Read More
 STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA MAOVU YA EX WAKE  PRITTY VISHY

STIVO SIMPLE BOY AFUNGUKA MAOVU YA EX WAKE PRITTY VISHY

Msanii Stivo Simple Boy ameingia kwenye headlines mara baada ya kuanika hadharani maovu ya mpenzi wake wa zamani Prity Vishy. Akipiga stori na podcast ya Oga Obinna Stivo ameibuka na kudai kuwa Pritty alikuwa na zaidi ya wanaume 50 ambao alikuwa anatoka nao kimapenzi. Msanii huyo wa Men in Business amesema alikuwa tayari kufunga ndoa na Pritty Vishy lakini mrembo huyo alidinda kubadili mienendo yake ya kutembea wanaume mbali mbali, jambo ambalo anadai lilimpelekea kuvunja uhusiano wake na mrembo huyo. “Mimi nilikuwa namuambia kama ananipenda ukweli, awachane na hizi vitu zake na akuwe na mtu mmoja tufunge ndoa lakini hakuwa anaelewa.”, Amesema Stivo. Kauli ya hitmaker huyo wa ngoma ya “Freshi Barida” imekuja mara ya Ex wake Pritty Vish kudai kuwa alimsaliti kimapenzi Stivo Simple Boy kwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine ambapo alienda mbali zaidi na kukiri kuwa alikuwa kwenye mahusiano na msanii huyo kwa ajili ya kupoteza muda.

Read More