UONGOZI WA MEN IN BUSINESS WAMTAMBULISHA STIVO THE SIMPLE BOY KAMA MSANII WAO MPYA
Lebo ya muziki ya Men in Business imemtambulisha rasmi Stivo The Simple Boy kama msanii wao mpya. Lebo hiyo imesema imesaini msanii huyo kwa mkataba wa miaka miwili ambapo watasimamia shughuli zake za muziki. Uongozi wa Men in Business umewataka wakenya waendelee kufuatilia kazi za Stivo The Simple Boy kwani kuanzia sasa atakuwa na muendelezo mzuru wa kuachia ngoma bila kupoa. Hata hivyo baada ya kutambulishwa kama msanii mpya wa MIB, Stivo The Simple Boy amewashukuru wakenya kwa upendo ambao wamemuonyesha tangu aanze muziki huku akiahidi kuwapa burudani zaidi. Utakumbuka Stivo The Simple Boy alikuwa akisamimiwa na lebo ya muziki ya Made In Kibera ambayo ilimtoa kimuziki lakini msanii huyo aliahamua kuigura uongozi huo baada ya kupora pesa zake alizokuwa anazichuma kupitia muziki wake
Read More