Suge Knight Adai Cheni ya Tupac Aliyonunua Drake Ni Bandia

Suge Knight Adai Cheni ya Tupac Aliyonunua Drake Ni Bandia

Aliyekuwa CEO wa Death Row Records, Suge Knight, ameibua madai makali akiwa jela kuhusu cheni ambayo rapa maarufu Drake alinunua kwa bei ya juu akiamini ilikuwa ya marehemu Tupac Shakur. Katika mahojiano aliyofanya akiwa gerezani, Suge alifichua kuwa cheni hiyo si halisi, akidai ni bandia (fake) na siyo ile aliyowahi kumpa Tupac kama zawadi enzi za uhai wake. Suge Knight alisema ana uhakika kwa sababu ndiye aliyemzawadia Tupac cheni ya asili, hivyo anajua kwa undani muonekano na maelezo yake ya kweli. Kwa kauli yake, anakanusha vikali uhalali wa cheni iliyouzwa kwa Drake, jambo linalotilia shaka historia ya thamani inayodaiwa kuambatana nayo. Kwa mujibu wa taarifa, Drake alinunua cheni hiyo kupitia Alexander Bitar, mtafutaji na muuzaji maarufu wa bidhaa za kihistoria, kwa gharama inayokadiriwa kuanzia $500,000 au zaidi. Cheni hiyo, yenye nembo ya Death Row, imekuwa ikihusishwa moja kwa moja na Tupac kutokana na picha na video zake maarufu akiivaa.

Read More
 Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Msanii wa R&B na mfanyabiashara Ray J ameibuka kwa hasira na kumshambulia vikali Suge Knight baada ya madai ya kushangaza aliyoyatoa kwenye kipindi cha televisheni cha Piers Morgan, ambapo Suge alisema kuwa Ray J na Diddy walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Madai haya yamezua hisia kali kwa Ray J na mashabiki wake. Ray J, ambaye awali alikuwa akimheshimu Rais huyo wa zamani wa Death Row Records, na kumtetea, alisema amevunjika moyo na kauli hizo zisizo na msingi. Alidai kuwa Suge amemshambulia kwa njia chafu na kuonyesha tabia ya kutojali, licha ya kuwa amekuwa akimuunga mkono katika nyakati ngumu. Aidha, Ray J alilalamikia namna Suge alivyoikosea heshima brand yake ya The Gaygency, inayosaidia wasanii wa jamii ya LGBTQIA+. Alisisitiza kuwa kuunga mkono jamii hiyo hakumaanishi kuwa yeye binafsi ni mpenzi wa jinsia moja, na ni aibu kwa Suge kutumia hilo kumshambulia. Ray J pia alimtuhumu Suge kuwa mtu anayeudhulumu watu wa karibu, ikiwemo wanaume na wanawake. Hadi sasa, Suge hajajibu madai hayo, huku mjadala ukiendelea kuenea mitandaoni kwa hisia kali kutoka kwa wafuasi wa pande zote.

Read More
 Suge Knight Amshauri Diddy Kufika Mahakamani na Kusema Ukweli Wake

Suge Knight Amshauri Diddy Kufika Mahakamani na Kusema Ukweli Wake

Rais wa zamani wa Death Row Records, Suge Knight, ambaye amekuwa mpinzani wa muda mrefu wa msanii na mfanyabiashara Sean “Diddy” Combs, amemtaka mwanamuziki huyo maarufu kufika kizimbani na kueleza ukweli wake katika kesi inayomkabili, akiamini kuwa hatua hiyo inaweza kuushawishi vizuri upande wa majaji. Katika mahojiano ya simu na Laura Coates wa CNN, Knight alisisitiza umuhimu wa Combs kujionyesha kama binadamu wa kawaida.  “Ninaamini kama atasimama na kusema ukweli wake, basi atapata nafasi ya kuachiwa,” Knight alisema. “Kama Puffy atasema, ‘Nilikua natumia madawa ya kulevya. Sikuwa na udhibiti wa maisha yangu au nafsi yangu,’ basi ataweza kujihumanisha, na jopo la majaji linaweza kumuelewa.” Knight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela kwa kosa la kuua mtu kwa makusudi kupitia ajali ya gari mwaka 2015, alionya kuwa ukimya unaweza kuathiri kesi ya Combs. “Kama ataendelea kukaa kimya, itaonekana kama anaogopa ukweli. Anatakiwa kuwa na imani na Mungu, avae suruali zake, asimame na aseme ukweli wake,” alisema Knight. Sean “Diddy” Combs amekana mashtaka ya kupanga njama ya uhalifu (racketeering), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, na usafirishaji kwa nia ya ukahaba. Ikiwa atapatikana na hatia kwa mashtaka yote, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Read More