EDDY YAWE ATUHUMIWA KUMNYANYASA KINJISIA MSANII CHIPUKIZI UGANDA
Msanii Eddy Yaawe ameingia kwenye headlines mtandaoni mara baada ya msanii mwenye asili ya Uganda anayeishi nchini Denmark kumkashifu kwa madai ya kuhujumu shughuli zake za muziki. Msanii huyo anayefahamika kwa jina la Sumaya Sheebah amefunguka na kudai kuwa Eddy Yawe aliuuza wimbo wake kwa mtu mwingine bila ridhaa yake alipokataa kumpa rushwa ya ngono. Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya kukubali kulipia gharama zote za kuandaa na kutayarishaji video ya wimbo huo, Eddy Yawe aliamua kufanya kazi hiyo na msanii mwingine aitwaye TYBA. Sheebah amedai alikutana na bosi huyo wa Dream Studios mwaka wa 2017 huko Copenhagen ambako walitia sahihi mkataba wa kufanya kazi pamoja ila tangu kipindi hicho amekuwa akimpa ahadi za uongo Hata hivyo Eddy Yawe amesalia kimya kuhusu tuhuma hizo za kutaka kimnyanyasa kinjisia binti huyo.
Read More