Susumila aachia rasmi EP yake mpya

Susumila aachia rasmi EP yake mpya

Mwanamuziki kutoka Pwani ya Kenya Susumila ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Lost Files. EP hiyo ina jumla ya ngoma saba za moto huku ikiwa kollabo 6 kutoka kwa wakali kama Jollie, Totti, Jacky Chant, Mejja, Jay Crack na Mr. Bado. Lost Files EP ambayo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya ina ngoma kama Mambo, Kiuno, Tetereka, Switi, Niache Niende,na Pweza. Utakumbuka mara ya mwisho Susumila kutubariki na kazi mpya ilikuwa ni mwaka wa 2021 alipoachia King is King EP iliyokuwa na jumla ya nyimbo 4 za moto.

Read More
 Susumila adokeza ujio wa EP mpya

Susumila adokeza ujio wa EP mpya

Mwanamuziki mkongwe nchini Susumila ametangaza ujio wa EP yake mpya aliyoipa jina la Lost Files. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema EP hiyo ni mkusanyiko wa nyimbo alizozifanya miaka kadhaa nyuma ambazo kwa njia moja au nyingine hakufanikiwa kuziachia kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake. Aidha Msanii huyo kutoka 001 Music amesema amechukua hatua ya kuachia EP hiyo kwa ajili ya kupisha njia ya kutoa kazi zake mpya kwa mwaka 2023. “Lost Files Ep ni kazi ambazo nimezifanya kwa miaka kadhaa ambazo kwa sababu moja ama nyingine hazikutoka now kabla nianze kutoa projects ambazo nimeanza kuzifanya huu mwaka nimeamua kuziachia ili tuanze upya tukisonga mbele links ndio hizo zinakuja polepole na shukran in advance Happy New Year…”, Aliandika. Hata hivyo hajaweka wazi idadi ya ngoma zinazopatikana kwenye Lost Files EP wala wasanii aliowashirikisha ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka mara ya mwisho Susumila kutubariki na kazi mpya ilikuwa ni mwaka wa 2021 alipoachia King is King EP iliyokuwa na jumla ya nyimbo 4 za moto.

Read More
 SUSUMILA AKANUSHA KUSTAAFU MUZIKI

SUSUMILA AKANUSHA KUSTAAFU MUZIKI

Msani nyota nchini Susumila amekanusha kustaafu muziki baada ya kuonekana kutokuwa na mazoea ya kuachia kazi mfululizo bila kupoa kama kipindi cha nyuma. Akizungumza na Captain Nyota Susumila amesema madai hayo sio ya kweli huku akisisitiza kuwa ataendelea kufanya muziki hadi mwisho wa dunia. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Siasa duni” amesema kwa sasa ashindani na msanii yeyote kwa kuwa tayari ana jina kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya, hivyo ataachia nyimbo zake bila kushurutishwa na mtu yeyote. Sanjari na hilo Susumila ambaye amekaa kwenye tasnia ya muziki nchini kwa kipindi cha miaka 15, amedokeza ujio wa kolabo yake na staa kutoka Nigeria Davido kwa kusema kuwa kwa sasa wanaendelea na mazungumzo kufanikisha kolabo hiyo. Utakumbuka Susumila juzi kati alidai kuwa ataachia kazi yeyote ya muziki wakati huu taifa la Kenya linaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kwa sababu ya wimbi la siasa.

Read More
 SUSUMILA AWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA KUPITIA WIMBO WAKE WA SONONA

SUSUMILA AWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA KUPITIA WIMBO WAKE WA SONONA

Januari 15 mwaka wa 2020 Staa wa muziki nchini Susumila alitubariki na singo inayokwenda kwa Sonona akiwa ameshirikisha msanii wa Bongofleva Mbosso. Goods news ni kwamba Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya streams millioni 1.5 kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay Kenya. Licha ya wimbo wa Sonona kufanya vizuri kwenye mtandao wa Boomplay,wimbo pia unazidi kupata mapokezi mazuri kwenye mtandao wa youtube kwani ndani ya kipindi cha miaka miwili imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara millioni 13.8 kwenye mtandao huo. Ikumbukwe Sonona ni singo ya kwanza kwa mtu mzima Susumila kufanya kazi na msanii wa lebo ya muziki ya WCB, ya pili ilikuwa ni Warembo wa Mombasa aliyomshirikisha Lava Lava.

Read More