Azawi Afichua Kuwekeza Milioni 24 Kurekebisha Meno

Azawi Afichua Kuwekeza Milioni 24 Kurekebisha Meno

Mwanamuziki wa Uganda, Azawi , amefunguka kuhusu uwekezaji mkubwa alioufanya kuboresha tabasamu lake, baada ya kupata mafanikio makubwa chini ya lebo ya Swangz Avenue. Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji wa YouTube, Kasuku, Azawi alieleza kuwa alitumia kiasi cha shilingi milioni 24 za Uganda (UGX) kurekebisha tatizo la meno lililosababishwa na ajali aliyopata alipokuwa katika umri mdogo. Msanii huyo alisema alianguka na kuvunjika taya, hali iliyosababisha mapengo yaliyoathiri muonekano wake kwa muda mrefu.  “Sikuwa na uwezo wa kuyarekebisha zamani, lakini baada ya kupata mafanikio kupitia muziki wangu chini ya Swangz Avenue, niliamua kuweka hilo suala sawa. Ilikuwa ni hatua ya binafsi na ya muhimu kwangu,” alisema Azawi. Katika mahojiano hayo, Azawi pia aligusia maisha yake ya kimapenzi, akifichua kuwa awali alikuwa katika mahusiano ya muda mfupi, lakini sasa yuko tayari kutulia. Kwa utani, alieleza kuwa hupendelea wanaume warefu na wanene, akisema haavutiiwi na wanaume wenye misuli (six-packs). Azawi anaendelea kung’ara katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki, na sasa si tu kwa sauti yake ya kipekee, bali pia kwa tabasamu linaloendana na jina lake kubwa. Swangz Avenue ilimsaini Azawi mwaka 2019 na kumtambulisha rasmi kwa umma tarehe 31 Oktoba mwaka huo. Tangu wakati huo, amejizolea umaarufu kwa nyimbo kama ‘Lo Fit’, ‘Masavu’, ‘Party Mood’, ‘Majje’, ‘Quinamino’, na ‘Ku Sure’.

Read More
 Azawi Kutumia Muziki Kupaza Sauti za Waganda Walionyimwa Haki

Azawi Kutumia Muziki Kupaza Sauti za Waganda Walionyimwa Haki

Mwanamuziki wa Uganda, Priscilla Zawedde maarufu kama Azawi, ameweka wazi dhamira yake ya kutumia muziki kama chombo cha kupaza sauti dhidi ya dhuluma na ukosefu wa haki nchini mwake. Hii ni baada ya takriban miaka miwili ya kuikosoa serikali hadharani kupitia majukwaa mbalimbali. Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Uganda, Azawi alieleza kuwa yupo mbioni kuingia studio kurekodi nyimbo za mapinduzi zenye ujumbe mzito unaoelezea machungu na hali halisi ya wananchi wa kawaida. “Nataka kuonesha maumivu ya Waganda wengi kupitia muziki wangu,” alisema Azawi. “Nafanya kazi juu ya hilo, na label yangu Swangz Avenue wanaheshimu maoni na mtazamo wangu.” Akiwa chini ya usimamizi wa lebo ya Swangz Avenue, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Talking Stage” alisisitiza kuwa hana hofu ya kupoteza nafasi yake kwenye lebo hiyo, endapo msimamo wake wa kisanii hautaungwa mkono. “Ikiwa hawatataka kufanya kazi nami kwa sababu ya nyimbo hizo, ni sawa tu. Nitajiondoa,” alisema kwa msimamo thabiti. Azawi anaelekea kufungua ukurasa mpya wa muziki wenye uzito wa kijamii na kisiasa, hatua ambayo huenda ikamuweka kwenye mgongano na serikali au hata wasimamizi wake wa kazi za usanii lakini pia inaweza kumweka katika nafasi ya kipekee kama msanii anayesimama kwa ajili ya watu wake. Hata hivyo mashabiki wake wameonyesha msisimko mkubwa mtandaoni, wakimpongeza kwa ujasiri na nia ya kutumia muziki kama silaha ya kupigania haki na kuunganisha jamii.

Read More
 PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

Promota wa Uganda wanayoishi mjini London Maama Africa ametishia kuhakikisha kuwa waimbaji wote wa Swangz Avenue wamepigwa marufuku kusafiri hadi London, lebo hiyo isipomlipa fidia ya euro 65000. Promota hao anadai kuwa alilipa Euro 5000 ili Winnie Nwagi atumbuize London lakini siku ya tukio, Nwagi pamoja na Fik Fameika walikataa kutoa burudani kwa mashabiki hadi usiku wa manane wakati walipotumbuiza nyimbo chache. Lakini pia wasanii hao walivunja mkataba na kutumbuiza kwenye shoo nyingine iliyopewa jina la “Chill and Grill” kwa kutumia kibali chake cha kazi, kitu ambacho anaona si cha kingwana. “Nataka kuwafundisha uweledi waimbaji wa Uganda. Nililipa na kugharamia kila kitu kwa Winnie Nwagi, lakini alienda mbali zaidi na kutumbuiza katika hafla nyingine bila idhini yangu,” alisema katika mahojiano na MwanaYouTube. Promota hao wameongeza, “Aliimba nyimbo chache tu baada ya kuchelewa kufika. Nimeiandikia Swangz avenue kuhusu kitendo hicho na ninatarajia jibu kabla ya Jumatatu la sivyo nitahakikisha kuwa wasanii wake wanapigwa marufuku kutumbuiza London.” Hata hivyo Maama Africa wanahusisha kuporomoka kwa onyesho hilo na vitendo visivyo vya kitaaluma vya Winnie Nwagi.

Read More
 VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka ametia saini mktaba mpya na lebo ya muziki ya Swangz Avenue ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu msanii mwenzake Winnie Nwagi aongeze mkataba wake na lebo hiyo. Vinka ameweka wazi habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akitia wino mkataba wake wa miaka 5 na lebo hiyo kwenye hafla iliyoshuhudiwa na Afisa mkuu mtendaji wa Swangz Avenue Julius Kyazze pamoja na wakili wake Joel Plus. Kulingana na Swangz Avenue Vinka bado ni msanii wa Sony music Africa ambaye ana mkataba mrefu nao ila swangz avenue itabaki kuwa uongozi wake kwa niaba ya Sony music. Lakini pia lebo hiyo imekanusha taarifa za kuwatema wasanii wake wakongwe baada ya kuwasaini wasanii wapya kama Zafarah na Azawi. Swangz avenue imekuwa ikisimamia muziki wa Vinka tangu mwaka wa 2016 na mwaka wa 2018 Vinka alisaini mkataba na sony music. Utakumbuka mpaka sasa Swangz Avenue ina jumla ya wasanii 4 ambao ni Winnie Nwagi, Azawi, Vinka na Zafaran ambaye alisainiwa majuzi na lebo hiyo.

Read More