Wasanii Waathirika na Marufuku ya Betting, Ssaru Asema Wameachwa Bila Kipato

Wasanii Waathirika na Marufuku ya Betting, Ssaru Asema Wameachwa Bila Kipato

Mwanamuziki wa gengetone Sylvia Ssaru, maarufu kama Ssaru, amefunguka kwa uchungu kuhusu athari za marufuku ya Bodi ya Kudhibiti Kamari nchini Kenya (BCLB) dhidi ya matangazo ya betting kupitia influencers na wasanii. Akizungumza na SPM Buzz katika mahojiano maalum, Ssaru alisema marufuku hiyo imeathiri moja kwa moja kipato chake na cha wasanii wengine waliokuwa wakitegemea mikataba ya ubalozi kutoka kwa kampuni za kubashiri. “Ni kama tumetolewa nyama kwa mdomo. Hapa ndo tunatoanga rent, pesa za video. Kuna influencer labda hii ndo deal yake ya kwanza, na sasa they consider themselves jobless,” alisema. Kauli ya Ssaru imekuja siku chache tu baada ya BCLB kutoa agizo rasmi likipiga marufuku kampuni za kubashiri kutumia influencers, wanablogu, na majukwaa ya mitandao ya kijamii kama sehemu ya mikakati yao ya matangazo. Katika waraka uliotumwa kwa kampuni mbalimbali, BCLB ilisema kuwa matumizi ya watu maarufu katika kuchochea tabia ya kubashiri ni kinyume na sheria na inahatarisha kizazi cha sasa, hasa vijana. Hii imeacha pengo kubwa kwa wasanii na maudhui wa dijitali ambao walikuwa wakitegemea kampeni hizo kama chanzo mbadala cha mapato katika tasnia isiyo na uhakika wa kipato wa kila siku.

Read More
 SYLVIA SSARU ATANGAZA UJIO MPYA MWAKANI

SYLVIA SSARU ATANGAZA UJIO MPYA MWAKANI

Wakati tukielekea ukingoni kabisa mwa mwaka 2021, na kuukaribisha mwaka 2022, Female rapper kutoka Kenya anayetajwa kuwa na sauti ya kipekee yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni, mwanadada Sylvia Ssaru ameweka wazi kuwa  mwakani ataachia album yake mpya. Lengo Ssaru ni kukata kiu ya mashabiki wake ambao wanatamani kuisikia sauti ya mwimbaji huyo hodari nchini  ikiwapa burudani ya kipekee. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea album yake mpya ambayo kwa mujibu wake itatoka rasmi mwanzo kabisa mwa mwaka mwa. Lakini pia amedokeza kwamba mwaka wa 2022 atakuwa moja kati ya wasanii watakaosainiwa na lebo ya seven hub creative ambayo inamsimamia msanii nadia mukami. Sylvia Ssaru ametoa taarifa hiyo mara baada ya kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wamempa kwenye muziki wake na kufanya kuwa miongoni mwa wasanii wa kike waliosikilizwa zaidi nchin kwenyew mtandao wa BoomPlay Kenyalicha ya kutoachia kazi nyingi mwaka huu.

Read More