T.I afunguka kuhusu mienendo ya mwanaye King Harris
Rapa kutoka nchini Marekani T.I. amefunguka kuhusu mwenendo wa mwanaye King Harris ambaye kipindi cha hivi karibuni amekuwa akikosolewa kwa kuwa na tabia mbaya mbele ya Jamii. Kwenye mahojiano mapya na Shannon Sharpe wiki hii, T.I. amemzungumzia King Harris na kumtetea kwa kusema βSisi kama wazazi, kati ya watoto wetu wote, tunao watoto waovu na wasiosikia. Nampenda licha ya yote ambayo anapitia, ni Kijana mzuri lakini vyombo vya habari haviongelei mambo mazuri, siku zote wanaanika maovu tu.β Rapa huyo amesema kwamba, mwanaye huyo ataishia gerezani kama hataamua kubadili tabia yake. Kama utakumbuka Septemba mwaka 2022, King Harris alikamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani ambapo alikutwa na kosa la kutovaa mkanda wakati akiendesha gari, ukiacha makosa mengine kama la kuwahi kumpiga muhudumu wa mgahawa mmoja Jijini Atlanta.
Read More