Taylor Swift na Travis Kelce Watangaza Rasmi Uchumba Wao

Taylor Swift na Travis Kelce Watangaza Rasmi Uchumba Wao

Msanii maarufu wa muziki wa pop, Taylor Swift, na nyota wa NFL kutoka timu ya Kansas City Chiefs, Travis Kelce, wametangaza rasmi uchumba wao juzi Agosti 26, 2025. Kupitia kurasa zao za Instagram, wawili hao wamechapisha picha wakionekana katika dimbwi zito la mapenzi. Katika maelezo ya picha hizo, waliandika kwa ucheshi, “Mwalimu wako wa Kiingereza na mwalimu wako wa mazoezi ya viungo wanafunga ndoa.” Kauli hiyo ya kifurushi cha maneno imeonyesha upekee wa uhusiano wao na kuleta msisimko zaidi kwa mashabiki wanaowafuatilia. Uhusiano wao ulianza mwaka 2023, baada ya Kelce kufichua kwenye podcast kuwa alijaribu kumpa Swift bangili yenye namba yake ya simu wakati wa tamasha lake la Eras Tour, ingawa hakufanikiwa. Baada ya hapo, wawili hao walianza kuonekana mara kwa mara pamoja kwenye michezo ya Kansas City Chiefs, ikiwemo Super Bowl, na hata walishiriki pamoja katika kipindi maarufu cha “Saturday Night Live.” Taylor Swift pia alionyesha dalili za uhusiano wao kupitia albamu yake ya mwaka 2024, The Tortured Poets Department, hasa katika nyimbo kama “The Alchemy” na “So High School” ambazo zilionekana kumrejelea mpenzi wake. Hata hivyo, tarehe rasmi ya harusi bado haijatangazwa, lakini mashabiki wao wamefurika kwenye mitandao ya kijamii kuwatumia pongezi na kuonyesha furaha kwa hatua hii mpya katika maisha ya wawili hao maarufu

Read More
 Taylor Swift Aandika Historia kwa Kurejesha Haki za Muziki Wake

Taylor Swift Aandika Historia kwa Kurejesha Haki za Muziki Wake

Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Taylor Swift, ametangaza rasmi kwamba amepata tena umiliki rasmi kazi zake za awali, hatua kubwa inayohitimisha miaka ya mapambano kuhusu haki ya umiliki wa kazi za wasanii. Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, Taylor alieleza furaha yake baada ya kurejesha umiliki wa albamu zake sita za mwanzo, ambazo awali zilikuwa chini ya lebo ya Big Machine. Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Swift aliwashukuru kwa uungwaji mkono waliompa katika kipindi chote cha changamoto. “Sasa ninamiliki muziki wangu. Asante kwa kusimama nami, safari hii haingekuwa na maana bila ninyi,” aliandika. Ameeleza kuwa hatua hii si tu ya kihistoria binafsi, bali ni mfano kwa wasanii wengine kuhusu umuhimu wa kumiliki kazi zao. “Hili ni jambo kubwa sana kwangu na kwa kila msanii anayepigania haki zake,” aliandika Taylor Taylor Swift sasa anamiliki kikamilifu albamu zake maarufu kama Fearless, Speak Now, Red, 1989, Taylor Swift (debut), na Reputation ambazo zilimjengea jina kubwa kimataifa. Wengi wa mashabiki wake wamesherehekea ushindi huu kama hatua ya haki na mafanikio dhidi ya mfumo wa muziki unaowanyima wasanii udhibiti wa kazi zao. Mnamo mwaka 2019, lebo ya muziki ya Big Machine iliuza katalogi yake ya muziki kwa meneja wa muziki Scooter Braun, ambaye baadaye aliuzia kampuni ya uwekezaji ya Shamrock Capital  bila ridhaa wala ushiriki wa Swift. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa kimataifa kuhusu haki za wasanii katika tasnia ya muziki, huku Taylor akichukua hatua ya kurekodi upya albamu zake ili kupata tena udhibiti wa kisheria.

Read More