Teacher Wanjiku Alalamikia Usafi Duni Kwenye Vituo vya Mafuta Kenya
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Teacher Wanjiku, ameibua malalamiko dhidi ya wamiliki wa vituo vya mafuta kufuatia hali mbaya ya usafi kwenye vyoo vyao. Kupitia ujumbe wake, Wanjiku ameeleza kuchoshwa na hali duni ya usafi katika baadhi ya vituo vya mafuta jijini Nairobi, akisema kwamba licha ya wateja wao kununua bidhaa na huduma, wengi wa wamiliki hao wamepuuza jukumu la kuhakikisha vyoo vinabaki safi na salama kutumika. Aidha, ameshauri wamiliki wa vituo hivyo kutafuta suluhu ya kudumu kwa kuanza kutoza ada ndogo kwa wateja wanaotumia vyoo, ili fedha hizo zitumike kugharamia usafi. Wanjiku amesema alijikuta kwenye hali ya kudhalilishwa baada ya kutumia choo katika kituo kimoja jijini Nairobi, na kusisitiza kuwa suala la usafi linapaswa kupewa kipaumbele ili kuenzi utu wa binadamu na kulinda afya za wananchi.
Read More