RAPPER TEKASHI 69 ATANGAZA UJIO WAKE MPYA

RAPPER TEKASHI 69 ATANGAZA UJIO WAKE MPYA

Rapper mtukutu kutoka nchini Marekani, Tekashi 69  ametangaza ujio wake mpya mara baada ya kutajwa kupata matatizo ya akili kutokana na kufilisika kiuchumi. 69 ambaye anajitamba kama Mfalme wa jiji la New York  ameShare kionjo cha video ya wimbo wake mpya alioutaja kutoka tarehe 15 mwezi huu na kueleza kuwa apishwe njia kwa ujio wake huu wa sasa kwa kuwa ni wakishindo. Rapper huyo anakumbukwa kwa smash hit yake ya Gooba yenye watazamaji million 781 kwenye mtandao wa Youtube, Wimbo huo ulitoka mwezi Mei mwaka 2020 na alifanya mara baada ya kutoka jela na kutumikia kifungo cha ndani

Read More
 RAPPER KUTOKA MAREKANI TEKASHI 69 AKIRI KUFILISIKA KIUCHUMI

RAPPER KUTOKA MAREKANI TEKASHI 69 AKIRI KUFILISIKA KIUCHUMI

Rapa kutoka marekani Tekashi 69 ameripotiwa kufulia kiuchumi hii ni baada ya kuomba mahakama imuonee huruma kutokana na hali mbaya ya kiuchumi anayopitia kwa sasa. Kuhusika kwake na tukio la wizi la mwaka wa 2018 kunamfanya rapa huyo kulipa fidia ndefu ambayo anahofu kuwa itammaliza kabisa kiuchumi. Kwa mujibu wa mtandao wa Complex, kupitia hati iliyosainiwa Machi 7 mwaka huu, Tekashi ameeleza kuwa ana watoto wadogo wawili na mama yao wanaomtegemea. Mkali huyo kutoka Brooklyn, anatajwa kuwa anapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na kutokuwa na Record’ Deal na kampuni yoyote huku pia ripoti zikidai kuwa hata katika matamasha mengi yanayofanyika mwaka huu ajapokea Bookings. Lakini pia dili lake na kampuni iliyokuwa ikimsimamia kimuziki ya Ten Thousand Project limekwisha rasmi nwezi uliopita na hawajasaini ten

Read More
 TEKASHI 69 ADUKULIWA AKAUNTI YAKE YA SPOTIFY

TEKASHI 69 ADUKULIWA AKAUNTI YAKE YA SPOTIFY

Akaunti ya Spotify ya Rapa Tekashi 69 kutoka Marekani imedukuliwa (Hacked)  na wadukuzi. Hii imekuja mara baada ya ghafla kubadilishwa kwa Profile Pic (DP) kwenye akaunti yake hiyo na kuwekwa picha ya Rapa Trippie Red na Lil Durk. Sio hayo tu  Bio ya rapa huyo pia imebadilishwa ambapo kwa wale waliofikia akaunti hiyo kwa muda huo walikutana na ujumbe ulioandikwa kuwa Tekashi 69 amekuwa akiishi kwa kutamani kuja kuwa kama rapa Trippie Red na Lil Durk. Mashabiki wa Trippie Red na Lil Durk  wametajwa kuhusika na udukuzi huo ikizingatiwa kuwa Tekashi 69 ana bifu na marapa hao wawili.

Read More