6ix9ine Akiri Kumiliki Madawa ya Kulevya, Hukumu Yasubiriwa Septemba
Rapa wa Marekani, Tekashi 6ix9ine, amekiri makosa ya kumiliki madawa ya kulevya kufuatia msako uliofanywa katika nyumba yake mjini Miami mwezi Machi mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, 6ix9ine alikiri mbele ya jaji kuwa alikuwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na MDMA (ecstasy), jambo ambalo linakiuka masharti ya probation aliyowekewa baada ya kesi yake ya mwaka 2018 inayohusiana na kundi la uhalifu la Nine Trey Gangsta Bloods. Msako huo wa Machi 2025 uliendeshwa na polisi wa Miami baada ya kupata taarifa za uhusiano wa rapa huyo na shughuli za uhalifu. Madawa hayo yalipatikana kwenye nyumba yake, na uchunguzi zaidi ukaonesha uvunjifu wa masharti ya muda wake wa majaribio (probation). Mahakama imepanga kutoa hukumu ya kesi hiyo mwezi Septemba 2025, huku wengi wakisubiri kuona iwapo 6ix9ine atapewa kifungo cha gerezani au adhabu mbadala. Kesi hii inaongeza msururu wa matatizo ya kisheria yanayomkabili rapa huyo, ambaye tangu afungue ukurasa mpya baada ya kutoa ushahidi dhidi ya wanachama wa genge la Nine Trey, amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa matukio ya utata.
Read More