Roboti wa Tesla “Optimus” Aonyesha Uwezo wa Kushangaza Katika Kucheza Muziki Kama Mwanadamu
Katika hatua nyingine ya kuvutia katika maendeleo ya teknolojia ya roboti, Bilionea Elon Musk ametoa onyesho jipya la roboti wa kampuni ya Tesla, anayejulikana kama Optimus. Kupitia video iliyosambazwa mitandaoni, roboti huyo ameonekana akicheza aina mbalimbali za muziki kwa ustadi wa kushangaza, akionyesha uwezo wa kufanya dance moves zinazofanana na za mwanadamu wa kawaida. Roboti huyo, ambaye awali alizinduliwa kama sehemu ya ndoto ya Tesla kuunda roboti wa kusaidia kazi mbalimbali, sasa amepewa uwezo wa kutambua sauti, kuchanganua midundo ya muziki, na kuratibu harakati zake kwa ufanisi wa hali ya juu. Katika video hiyo, Optimus anaonekana akijibu mabadiliko ya midundo ya muziki kwa hatua sahihi, jambo linalodhihirisha maendeleo makubwa katika mfumo wa AI (Artificial Intelligence) unaomwendesha. Kwa mujibu wa Musk, uwezo huu wa Optimus kucheza muziki si burudani tu, bali pia ni sehemu ya majaribio ya kufanya roboti huyo aweze kuelewa mazingira yake vizuri zaidi kupitia mchanganyiko wa sauti, mwonekano, na mwendo. Hii inaashiria kuwa Tesla inalenga zaidi kazi za kawaida kama kubeba mizigo au kusaidia nyumbani na ujio wa rboti hiyo inalenga kurahisisha zaidi kazi za binadamu Hatua hii mpya inachochea mjadala mpana kuhusu mustakabali wa roboti katika maisha ya kila siku, huku wengine wakijiuliza ni lini tutaweza kuwa na wasaidizi wa nyumbani wanaojua hata kucheza nasi.
Read More