Bien Aime Afafanua Msimamo Wake Kuhusu Ndoa ya Wake Wengi

Bien Aime Afafanua Msimamo Wake Kuhusu Ndoa ya Wake Wengi

Mwanamuziki maarufu wa kundi la Sauti Sol, Bien Aime Baraza, amefunguka kuhusu msimamo wake kuhusu ndoa za wake wengi, akisema hana mpango wa kuoa zaidi ya mke mmoja. Akihojiwa kwenye kipindi cha The Breakfast Club, Bien alieleza kuwa licha ya kukulia kwenye familia ya wake wengi, yeye ana mtazamo tofauti. “Ninatoka katika familia ya wake wengi, baba yangu ana watoto kumi kutoka kwa wanawake sita tofauti. Mimi ndiye wa mwisho kati ya hao kumi,” alisema Bien. Bien alisema uzoefu huo wa kifamilia umemfundisha mengi kuhusu mahusiano, na ndio maana amejiwekea msimamo wa kutotaka kuoa wake wengi. Mbali na hayo, Bien pia alisimulia changamoto alizopitia alipokuwa akitafuta kuku hai kwa ajili ya kipindi cha On The Radar kilichorekodiwa New York. Kwa mujibu wa msanii huyo, sheria kali za wanyama katika jiji hilo zilimuweka kwenye wakati mgumu, kwani wauzaji wengi walikataa kumuuzia kuku huyo.  “Nililazimika kuendesha gari kwa zaidi ya saa moja hadi Pennsylvania ili kupata kuku hai. New York ni ngumu sana kwa hilo,” alisema Bien. Kauli hizo zimeendelea kumweka Bien katika uangalizi wa vyombo vya habari, huku mashabiki wakifurahia uwazi wake na uhalisia wa maisha anayoshiriki.

Read More