ALBUM YA THE GAME YAUZA NAKALA 25,000 NDANI YA WIKI MOJA

ALBUM YA THE GAME YAUZA NAKALA 25,000 NDANI YA WIKI MOJA

Album ya The Game “Drillmatic” imeuza Jumla ya nakala 25,000 kwenye wiki yake ya kwanza sokoni. Album hiyo imechumpa hadi namba 10 kwenye chart za Billboard 200. Hii inakuwa Album ya 9 kwa The Game kuingia kwenye Top 10 ya Chart hizo za Album bora. Ni ongezeko la nakala 2,000 toka kwenye mauzo ya Album yake iliyopita “Born 2 Rap” ambayo iliuza nakala 23,000 kwenye wiki yake ya kwanza. Wengi wanahoji juu ya mauzo haya wakisema Muziki wa The Game umeporomoka sana, kuna haja ya kubadili staili au aachane kabisa na Muziki. Una maoni gani kuhusu hili, tuachie comment yako.

Read More
 THE GAME ADAI YEYE NDIYE RAPA BORA KULIKO EMINEM

THE GAME ADAI YEYE NDIYE RAPA BORA KULIKO EMINEM

Rapa kutoka Marekani The Game anaendelea kusisitiza kuwa yeye ni rapa bora kuliko Eminem. Kupitia podcast ya All the Smoke, The Game amesema kwamba Eminem ni Mwandishi mzuri lakini yeye ni bora kumliko Eminem. Sababu kuu ya The Game kufunguka hayo ni kwamba anaamini Eminem ni mkali wa kuandika na kuchana lakini muziki wake sio mkubwa kutokana na kutochezwa kwenye kumbi za starehe na mtaani, ambapo yeye amefanikwa kwa hilo. The Game ameendelea kufunguka kwamba wadau wa muziki hawakuwekeza hela kwenye muziki wake na hakupata support ambayo Eminem na 50 Cent wameipata, kama wangefanya hivyo kwake basi ingekuwa habari nyingine.

Read More
 THE GAME AKANUSHA MADAI YA KUMTUSI JAY Z BAADA YA KUNYIMWA NAFASI KWENYE SHOW YA SUPER BOWL 2022

THE GAME AKANUSHA MADAI YA KUMTUSI JAY Z BAADA YA KUNYIMWA NAFASI KWENYE SHOW YA SUPER BOWL 2022

Rapa kutoka Marekani The Game amekanusha taarifa zote ambazo zinadai kwamba alimtukana Jay-Z baada ya kumnyima nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022. Kupitia instagram page yake The Game amesema hana mtu yeyote wa kumsemea isipokuwa yeye mwenyewe. Hii imekuja kufuatia meneja wake Wack 100 kufunguka kwamba The Game alimtukana Jay-Z tusi zito “Suck My D*k” baada ya kunyimwa nafasi hiyo ya kutumbuiza. The Game anasema hakuzungumza na mtu yeyote kuhusu Jay-Z au show ya Super Bowl, na kwa upande wake ilikuwa ni show nzuri sana. Rapa huyo alienda mbali zaidi na kumsifia Jay-Z kwa kazi nzuri ya kuendelea kufungua milango, na ameahidi kumuunga mkono kwa kila kitu.

Read More
 KUMBE THE GAME ALIMTUPIA JAY Z MATUSI MAZITO BAADA YA KUMNYIMA NAFASI YA KUTUMBUIZA KWENYE SUPER BOWL 2022

KUMBE THE GAME ALIMTUPIA JAY Z MATUSI MAZITO BAADA YA KUMNYIMA NAFASI YA KUTUMBUIZA KWENYE SUPER BOWL 2022

Rapa The Game kutoka Marekani amekasirika sana baada ya kukosa nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022, Wiki iliyopita alitokwa mapovu na kusema 50 Cent hakustahili kupewa nafasi hiyo. Meneja wake aitwaye Wack 100 ameibuka na kutusanua makubwa ambayo hatuyafahamu nyuma ya pazia. Wack 100 amesema The Game alimtukana Jay-Z tusi zito “Suck My D**k” baada ya kumnyima nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya fainali hizo za mwaka huu. Utakumbuka Roc Nation ya Jay Z waliingia makubaliano na NFL kuwa waandaaji wa burudani kwenye Super Bowl 2022. Kinyongo baina ya wasanii hao kilianza mwaka 2005 baada ya The Game kudai kwamba alijibiwa vibaya na Jay-Z walipokutana kwenye mgahawa wa 40/40 mjini New York ambapo The Game alimuomba ushauri Jigga ya namna ya kudumu muda mrefu kwenye muziki.

Read More
 THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

Stori kubwa wiki hii kwenye burudani ni Super Bowl Half Time Show ambayo inatajwa kuwa ya kihistoria, lakini The Game ana malalamiko yake. Baada ya 50 Cent kupandishwa na kutumbuiza kama Guest Artist, Rapa The Game pamoja na timu yake wameonekana kutopenda uamuzi huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, The Game ame-share ujumbe uliowekwa na miongoni mwa memba kwenye timu yake, ambao unasema inakuaje wanampa 50 Cent hiyo nafasi na sio The Game? Game alistahili kuwepo kwenye Jukwaa hilo pia Kauli ya The Game imekuja mara baada ya Super Bowl 2022 Halftime Show kufunguliwa kwa perfomance ya Dr. Dre na Snoop Dogg kupitia ngoma ya “The Next Episode” na “California Love” ya Tupac Shakur, ambapo Rapa na mfanyabiashara 50 Cent alitokea kwenye dakika ya 3:10 kupiga performance ya kufa mtu na ngoma ya “In Da Club” na kuamsha shangwe la aina yake. Eminem ndiye alimpa mashavu 50 Cent kutumbuiza kwenye halftime ya Super Bowl 2022. Eminem ndiye alitoa wazo hilo na kupitishwa na Dre pamoja na wote ambao walikuwa kwenye orodha ya watumbuizaji rasmi. Ikumbukwe Mtayarishaji mkongwe  kutoka Marekani Dr. Dre alitumia shillingi millioni 795 za Kenya kwa ajili ya kutayarisha performance nzima ya Halftime kwenye fainali za Super Bowl 2022 zilizofanyika Februari 14 katika uga wa SoFi huko California. Dunia ilishuhudia Dr. Dre akiandika historia akiwa na wakali wa Hip Hop nchini Marekani; kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent na mwanadada Mary J Bridge.

Read More