Drake na The Weeknd wagoma kupeleka kazi zao Grammy

Drake na The Weeknd wagoma kupeleka kazi zao Grammy

Wanamuziki Drake na The Weeknd wameendelea kuziwekea mgomo Tuzo za Grammy, taarifa mpya zinasema wakali hao kutoka nchini Canada hawajawasilisha nyimbo zao kwa ajili ya kufikiriwa (Consideration) kwa tuzo za mwaka 2023. Album zao ‘Honestly, Nevermind’ na ‘Dawn FM’ hazijawasilishwa kwenye kipengele chochote cha tuzo hizo kwa mwaka 2023 sambamba na nyimbo zao Hit kama ‘Sticky’ na ‘Out Of Time.’ Kwa upande wa Drizzy, amekuwa kwenye mahusiano mabaya na Waandaaji wa tuzo hizo tangu mwaka 2017 baada ya kutoridhika na kipengele ambacho wimbo wake “Hotline Bling” iliwekwa. Mwaka Jana alitangaza kujitoa kwenye Tuzo hizo baada ya kutajwa kwenye vipengele viwili ambapo alitajwa kuwania Best Rap Album na Best Rap Performance. Si hayo tu, Drake pia alisimimama kumtetea The Weeknd ambaye mwaka Jana alikosekana kwenye kipengele chochote cha Tuzo za Grammy licha ya kuachia Album “After Hours” ambayo ilifanya vizuri sana.

Read More
 KAMPUNI YA UNIVERSAL MUSIC GROUP YAINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA THE WEEKND

KAMPUNI YA UNIVERSAL MUSIC GROUP YAINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA THE WEEKND

Kampuni ya Universal Music Group imetangaza dili lake la ushirikiano na Mwanamuziki kutoka Marekani The Weeknd. Dili hilo linahusisha usimamizi wa kurekodi kazi zake, uchapishaji bidhaa na masuala ya video. Makubaliano hayo hayataathiri uhusiano wa The Weeknd na kampuni ya ‘UMG’s Republic Records’ ambayo ndiyo kampuni na mshirika wake wa muda mrefu katika kazi zake haswa za muziki tangu mwaka 2012. Hata hivyo kampuni ya UMG inayosimamia chapa (brand) na bidhaa za rappa huyo, itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Weeknd na XO ili kupanua na kuendeleza biashara ya kimataifa, biashara ya mtandaoni na fursa za leseni za rejareja kuhusu miradi na matoleo yajayo.

Read More
 THE WEEKND ATISHIA KUJIONDOA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

THE WEEKND ATISHIA KUJIONDOA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

Mwanamuziki kutoka Canada The Weeknd ametishia kujiondoa kwenye orodha ya wasanii kinara ambao wametajwa kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella. Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six, The Weekd amedai kuwa hatotumbuiza kwenye tamasha la Coachella kama atalipwa shillingi billioni za Kenya ambazo Kanye west alipaswa kupewa. Kauli ya the Weeknd inakuja siku chache baada ya kutajwa na kundi la Swedish House Mafia kuwa watatumbuiza kwenye tamasha la Coachella, kuchukua nafasi ya rapa Kanye West ambaye alijiondoa kwenye orodha ya watumbuizaji kinara wa tamasha hilo. Tamasha la Coachella litaanza April 15 hadi 24  mwaka huu nchini Marekani.

Read More
 THE WEEKND ADOKEZA MPANGO WA KUBADILI JINA LA USANII

THE WEEKND ADOKEZA MPANGO WA KUBADILI JINA LA USANII

Mwanamuziki The Weeknd anafikiria kubadilisha jina lake la muziki na kutumia ‘Abel’ ambalo ni jina lake la kuzaliwa. The Weeknd amefunguka matamanio yake hayo kupitia ukurasa wa Twitter, huku akihamasishwa na Kanye West ambaye alibadili jina lake na kuwa YE. Mastaa kadhaa na mashabiki wa mkali huyo wameonesha kuunga mkono wazo hilo akiwemo mwimbaji John Legend. The Weeknd ambaye anafahamika kama Abel Makkonen Tesfaye alizaliwa Toronto Canada mwaka 1990. Wazazi wake ni raia wa Ethiopia ambao walikimbilia nchini Canada miaka ya 80.

Read More
 THE WEEKND AMPIKU JUSTIN BIEBER KWA IDADI YA LISTENERS WA MWEZI SPOTIFY

THE WEEKND AMPIKU JUSTIN BIEBER KWA IDADI YA LISTENERS WA MWEZI SPOTIFY

Mwanamuziki kutoka Canda The Weeknd ndiye Mwanamfalme wa Pop kwa sasa duniani. Msanii huyo amempindua Justin Bieber kwa kufikisha jumla ya wasikilizaji wa mwezi milioni 85.86 kwenye mtandao wa Spotify akimuangusha Justin bieber mwenye wasikilizaji milioni 83.86 Justin Bieber alikuwa amekalia kiti hicho kwa siku 190 mfululizo na kusimikwa taji la Prince of Pop. The Weeknd anaendelea kufanya vizuri na album yake mpya “Dawn FM” ambayo hadi sasa imesikilizwa zaidi ya mara milioni 750 kwenye Spotify.

Read More