Thee Pluto Akana Madai ya Kudate Mwanamke wa Kisomali

Thee Pluto Akana Madai ya Kudate Mwanamke wa Kisomali

YouTuber maarufu wa Kenya, Thee Pluto, amejitokeza kufafanua madai yaliyosambaa mitandaoni kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Kisomali. Akizungumza kupitia mitandao yake ya kijamii, Thee Pluto amesema kuwa si kila mtu anayepigwa naye picha au kuonekana naye hadharani ni mpenzi wake. Amesisitiza kuwa uvumi wa aina hiyo ni wa kupotosha na umekuwa ukiwaweka watu katika hali ya mkanganyiko kuhusu maisha yake ya kibinafsi. Thee Pluto, ambaye ni maarufu kwa majaribio yake ya uaminifu (loyalty tests) mitandaoni, ameomba mashabiki na wafuasi wake kutofautisha kati ya mahusiano ya kirafiki na kimapenzi, akiongeza kwamba si kila anayeonekana naye ana uhusiano wa kindoa naye.

Read More
 Thee Pluto Apokea YouTube Gold Play Button Kwa Subscribers Milioni Moja

Thee Pluto Apokea YouTube Gold Play Button Kwa Subscribers Milioni Moja

Mwanamitandao maarufu Thee Pluto ameendelea kuandika historia katika tasnia ya maudhui ya kidijitali baada ya kipindi chake cha Thee Pluto Show kufikisha zaidi ya subscribers milioni moja kwenye mtandao wa YouTube. Hatua hiyo imemfanya kutunukiwa tuzo ya heshima ya YouTube Gold Play Button, ikiwatambua waundaji wa maudhui wanaofikisha idadi hiyo kubwa ya subscribers. Thee Pluto, anayefahamika zaidi kwa vipindi vyake vya loyalty test ambavyo vimejipatia mashabiki wengi hususan vijana, alisherehekea mafanikio haya makubwa akiwa likizoni katika kisiwa cha Bali, Indonesia. Aliwashukuru mashabiki wake kwa mchango wao mkubwa katika safari yake, akisema bila wao mafanikio hayo yasingewezekana. Kwa mujibu wa takwimu za akaunti yake, Thee Pluto alijiunga na YouTube mnamo Januari 5, 2018, na kufikia sasa ameshapakia zaidi ya video 1,288, ambazo kwa pamoja zimeangaliwa zaidi ya mara 273 milioni. Hii ni ishara ya ushawishi wake mkubwa na nafasi yake katika soko la burudani mtandaoni. Kwa kutunukiwa Gold Play Button, Thee Pluto amejiunga na kundi dogo la waundaji maudhui wa Kenya waliovuka mipaka ya ndani na kuonyesha kuwa bidii, ubunifu na uthabiti vinaweza kufanikisha safari ya kimataifa kupitia jukwaa la YouTube.

Read More