Tiffy Dolly Ajibu Madai ya Kuishi Maisha ya Kuigiza
Mwanamitindo na mtayarishaji wa maudhui mtandaoni, Tiffy Dolly, amejibu vikali madai ya baadhi ya watu mitandaoni waliodai kuwa anaishi maisha ya kuigiza (fake lifestyle) baada ya kushiriki skrini inayomuonesha akiwa na salio la Ksh 590,000 kwenye akaunti yake ya M-Pesa. Baada ya kuchapisha picha hiyo, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walimshambulia kwa kusema kuwa anajaribu kuonyesha maisha ya kifahari yasiyo halisi. Hata hivyo, Tiffy Dolly hakusita kujibu, akisisitiza kuwa mafanikio yake ni halali na yanatokana na kazi yake ya kujituma kama content creator. Alisisitiza kuwa badala ya kukosoa, watu wanapaswa kujituma na kuzingatia maendeleo yao wenyewe. βKila mtu anapigania maisha yake kwa njia yake. Sina muda wa kudanganya watu kuhusu maisha yangu. Kazi yangu inanilipa vizuri, na sioni shida kusherehekea mafanikio yangu,β alisema Tiffy kupitia Instagram. Tukio hili limezua hisia mseto mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wake wakimuunga mkono kwa kusema kuwa ni kawaida kwa watu wenye mafanikio kukumbwa na chuki, hasa wanapokuwa wazi kuhusu mafanikio yao ya kifedha. Tiffy Dolly anaendelea kuwa miongoni mwa wanamitandao wa kijamii wanaofuatiliwa sana, huku akiendeleza harakati zake za kujenga chapa binafsi inayohusisha urembo, mtindo wa maisha na ujasiriamali wa kidijitali.
Read More