TIP SWIZZY AGOMA KUFANYA KOLABO NA WASANII WENZAKE

TIP SWIZZY AGOMA KUFANYA KOLABO NA WASANII WENZAKE

Msanii anayesuasua kwenye muziki nchini Uganda Tip Swizzy hataki tena kufanya kolabo na wasanii wengine baada ya kutimuliwa kwenye lebo ya muziki ya Big Talent Entertainment inayomilikiwa na Eddy Kenzo. Msanii  huyo amesema  aliwekeza miaka yake ya ujana kufanya kolabo na wasanii wenzake lakini mpaka sasa hazijamsaidia. Tip swizzy amedai hapokei tena mirahaba kutoka kwa nyimbo alizofanya na Eddy Kenzo. Akiwa kwenye lebo ya muziki ya Big Talent Entertainment, alishirikiana na Eddy Kenzo kwenye  wimbo uitwao “Boligo”, wimbo ambao baadaye ulikuja ukavuma sana nchini Uganda. Hata hivyo, Tip Swizzy aliigura lebo ya muziki ya  Big Talent Entertainment baada ya kuingia kwenye ugomvi wa pesa na bosi wake wa zamani Eddy Kenzo.

Read More