Drama Mpya! Tipsy Gee na Toxic Lyrikali Waendeleza Bifu Kali Mitandaoni
Tiktoker aliyegeukia muziki kutoka Kenya Tipsy Gee ameibua mjadala mitandaoni baada ya kumshusha wazi wazi Rapa Toxic Lyrikali, akimtuhumu kwa kujivunia views nyingi bila kuwa na ubora wa kweli kwenye muziki. Kwa mujibu wa Tipsy Gee, mafanikio ya kupata watazamaji wengi mtandaoni hayatoshi kuthibitisha kuwa msanii ndiye bora zaidi. Ametoa mfano wa wakali kama Bien na Nyashinski, akisema licha ya wao kutotegemea views pekee, wamejijengea heshima kubwa kutokana na kazi zenye ubora na ushawishi mkubwa katika muziki wa Kenya. Bifu kati ya wawili hao lilianza baada ya Toxic kukataa kufanya kolabo na Tipsy Gee, hali iliyochochea uhasama unaoendelea hadi sasa. Tangu wakati huo, Tipsy amekuwa akimtupia maneno makali mitandaoni, akimkosoa vikali kila mara. Hata hivyo Toxic amekuwa akimsisitizia mpinzani wake huyo aache kutumia jina lake kama kiki ya kutafuta umaarufu. Amesema kuwa Tipsy anapaswa kuonyesha uwezo wake kupitia muziki badala ya kutumia mitandao kushambulia wasanii.
Read More