Tiwa Savage Akana Tuhuma za Mahusiano ya Siri na Wizkid

Tiwa Savage Akana Tuhuma za Mahusiano ya Siri na Wizkid

Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria, Tiwa Savage, amekanusha uvumi ulioenea kwa muda mrefu kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Wizkid. Akizungumza katika mahojiano na The Breakfast Club, Tiwa Savage amesisitiza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote. Ameeleza kuwa hakuwahi kuwa kwenye mahusiano ya siri na Wizkid na kuongeza kwamba maneno hayo ni uvumi wa watu usio na msingi. Msanii huyo amefafanua kuwa madai hayo yalianza kuenea baada ya yeye kudaiwa kuwa kwenye uhusiano na mtu maarufu ambaye alitaka penzi lao libaki la siri. Hata hivyo, Tiwa amesema hana chochote cha kuficha na hakuwahi kushirikiana kimapenzi na Wizkid, bali walihusiana tu kwa sababu ya kazi za muziki. Tiwa Savage, ambaye ni mmoja wa wasanii wa kike wenye ushawishi mkubwa barani Afrika na duniani, ameongeza kwamba anataka mashabiki wake waendelee kumtambua kupitia kazi zake na mafanikio ya muziki badala ya skendo za maisha yake ya kibinafsi.

Read More
 Tiwa Savage Aweka Mipaka Mapya ya Mapenzi Mitandaoni

Tiwa Savage Aweka Mipaka Mapya ya Mapenzi Mitandaoni

Malkia wa muziki wa AfroBeats, Tiwa Savage, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kufichua vigezo anavyovitaka kwa mwanaume wa ndoto zake. Akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Tiwa alieleza kuwa hana mpenzi kwa sasa, na si kwa sababu kuna uhaba wa wanaume, bali ni kutokana na matarajio maalum aliyojiwekea. Kwa sasa, anatafuta mwanaume mwenye ndege binafsi (private jet), mwenye boti, na asiye na changamoto au drama zinazohusiana na wanawake wengine. Anaamini huenda vigezo hivyo vikawa sababu ya kutompata mtu anayemfaa hadi sasa. Kauli hiyo imezua mijadala mseto mitandaoni. Baadhi ya mashabiki wamepongeza msimamo wake kama ishara ya kujua thamani yake, huku wengine wakiona vigezo hivyo kuwa vya hali ya juu sana. Tiwa Savage, ambaye ameweka alama kubwa kwenye muziki wa Afrika na kimataifa, anaendelea kuwa mfano wa mwanamke jasiri, mwenye malengo na maamuzi thabiti hata linapokuja suala la mapenzi.

Read More
 TIWA SAVAGE AUZA TIKETI ZOTE ZA SHOW YAKE TORONTO

TIWA SAVAGE AUZA TIKETI ZOTE ZA SHOW YAKE TORONTO

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, msanii Tiwa Savage amethibitisha kumalizika (sold out) kwa tiketi zote katika Show yake itayofanyika Juni 19, katika ukumbi wa Longboat huko Toronto, Canada. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tiwa Savage ameandika ujumbe unaosomeka “We already sold out Toronto 💫💫💫💫 #WaterAndGarriTour. Ticket link for other cities in my bio ❤,” Show hiyo iliyopo ndani ya ziara yake ya Water & Garri itaanza rasmi Mei 15 huko jijini New York na itafanyika ndani ya miji 17 kwa kipindi cha miezi miwili. Hitmaker huyo wa ‘Somebod’s Son’ Tiwa Savage ambaye baadae mwaka huu anatarajiwa kuachia albamu yake mpya, ziara hii inakuwa ni ziara kubwa na ya kwanza kwake.

Read More
 TIWA SAVAGE ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI

TIWA SAVAGE ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI

Staa wa muziki kutoka Nigeria, msanii Tiwa Savage yupo mbioni kuweka historia kupitia ziara yake ya kimuziki iitwayo Water & Garri Tour atakayoifanya kwenye miji iliyopo Kaskazini mwa Marekani. Hitmaker huyo wa ‘Somebody’s Son’ ametaja ziara hiyo kuanza Mei 15 huko jijini New York na itafanyika ndani ya miji 17 kwa kipindi cha miezi miwili. Tiwa Savage ambaye anatarajiwa baadae mwaka huu kuachia albamu yake mpya, ziara hiyo inakuwa ziara kubwa na ya kwanza kwake kuifanya Marekani.

Read More
 TIWA SAVAGE AFUNGUKA JUU YA VIDEO YAKE YA NGONO ILIYOVUJA MTANDAONI

TIWA SAVAGE AFUNGUKA JUU YA VIDEO YAKE YA NGONO ILIYOVUJA MTANDAONI

Baada ya kutangaza mwenyewe kuvuja kwa mkanda wa Video yake ya ngono ikumuonesha akiwa n mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki wa kike kutoka nchini Nigeria Tiwa Savage sasa amebainisha kuwa hamtoweza kuziona tena video zake za ngono. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram na kauli aliyo izungumza wakati wa performance yake huko nchini Nigeria imebainisha hilo, huku baadhi ya watu wakiielezea kuwa ameitumia jambo hilo kama Kiki kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya wa Somebody’s Son alio mshirikisha msanii wa Marekani, Brandy.

Read More