Bifu Laibuka Kati ya Toxic Lyrikali na Tipsy Gee Mtandaoni
Rapa kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, ameonyesha kutoridhishwa na skit iliyosambaa mtandaoni ikimuonesha mwenzake Tipsy Gee akijifananisha kuwa na mafanikio makubwa zaidi. Katika skit hiyo, Tipsy anaonekana akiendesha gari huku waigizaji waliobandikwa majina ya Toxic na Fathermoh wakiendesha bodaboda, jambo lililotafsiriwa kama kejeli kwao. Kupitia Instagram Toxic amechukizwa na kejeli hiyo na kumtaka Tipsy kuacha mbwembwe na kurudi studio kutoa muziki. Amesema wazi kuwa Tipsy amekuwa akiendesha maigizo mtandaoni badala ya kufanya kazi ya muziki, akimtupia lawama kuwa amegeuka kuwa TikToker anayejali kiki kuliko kutoa ngoma mpya. Kauli ya Toxic imekuja mara baada ya Tipsy Gee, kumtolea uvivu, akidai kwamba licha ya Toxic kumpuuza, yeye ndiye msanii aliye na mafanikio zaidi japo amekaa kwenye tasnia kwa mwaka mmoja pekee.
Read More