Jini mkata kamba aingilia ndoa ya Kylie Jenner na Travis Scott

Jini mkata kamba aingilia ndoa ya Kylie Jenner na Travis Scott

Kylie Jenner na Travis Scott wameachana tena, chanzo cha karibu na wawili hao kimeripoti kwamba hata msimu huu wa Sikukuu wamesherehekea kila mmoja kivyake. Hii inakuwa mara ya pili kwa wapenzi hao kuachana, penzi lao liliwahi kuvunjika Oktoba 2019 na kurudiana tena Mei, 2021. Hata hivyo mitandao ya nchini Marekani inaeleza kwamba, Kylie na Travis wataendelea kushirikiana kwenye malezi ya watoto wao wawili, Stormi na wa Kiume (Wolf) waliyempata Februari mwaka 2022.

Read More
 Travis Scott na Kylie Jenner kubadilisha jina la mtoto wao

Travis Scott na Kylie Jenner kubadilisha jina la mtoto wao

Rapa kutoka Marekani Travis Scott na Baby Mama wake Kylie Jenner wanapanga kubadilisha Jina la mtoto wao wa kiume (Wolf Webster), wawili hao wanajuta kumpatia Jina hilo mtoto huyo wa pili ambaye ana umri wa miezi 8 sasa. Kwa mujibu wa Kylie kwenye Episode ya Keeping Up with The Kardashians, Jina hilo lilitolewa na Khloe Kardashian na kwa wakati huo alilipenda lakini punde tu baada ya kuliandika na kuangusha saini kwenye cheti cha Kuzaliwa, aliingia majuto ya kutamani kulibadilisha.

Read More
 TRAVIS SCOTT ATAJWA KUWA MSANII KINARA KATIKA TAMASHA LA DAY N VEGAS

TRAVIS SCOTT ATAJWA KUWA MSANII KINARA KATIKA TAMASHA LA DAY N VEGAS

Rapper Travis Scott ametajwa kuwa msanii Kinara katika tamasha la Day N Vegas ambalo litafanyika September 2 hadi 4 Jijini Las Vegas nchini Marekani. Hili linakuwa tamasha lake la kwanza nchini Marekani tangu Janga lililotokea kwenye tamasha lake la ‘Astroworld Festival’ mwaka 2021 na kuchukua maisha ya watu 10 na namba kubwa ya majeruhi. Travis Scott alikuwa ‘booked’ kutumbuiza katika tamasha la Day N Vegas mwaka Jana lakini waandaaji wa tamasha hilo ilibidi wamuondoe kwenye orodha kufuatia Janga hilo ambalo lililotokea kwenye tamasha lake wiki chache nyuma na kuteka hisia za watu wengi nchini Marekani.

Read More
 DIDDY AFUNGUKA KUMKINGIA KIFUA TRAVIS SCOTT KWENYE TUZO ZA BILLBOARD

DIDDY AFUNGUKA KUMKINGIA KIFUA TRAVIS SCOTT KWENYE TUZO ZA BILLBOARD

Mkongwe wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani P. Diddy anaendelea kuthibitisha kwa nini anajiita “LOVE”, amefunguka wazi kwamba ni yeye ndiye alimpambania Travis Scott kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye Tuzo za Billboard (BBMA’s) ambazo zitafanyika Mei 16 mwaka huu. “For the Billboard Music Awards this Sunday I made a request, I made a demand. I said ‘My brother Travis Scott has to perform. I’m executive producing, he has to perform,’ and NBC said ‘yes.’ It’s going down Sunday, Travis Scott will be performing… now that’s love.” amekaririwa Diddy ambaye ni Mtayarishaji Mkuu wa Tuzo hizo. Hii itakuwa show ya pili kwa mtu mzima Travis Scott kutumbuiza tangu onesho la Astroworld ambalo lilipelekea vifo vya watu 10 na wengine 4,900 kujeruhiwa.

Read More
 RAPA TRAVIS SCOTT MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

RAPA TRAVIS SCOTT MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Marekani Travis Scott ameendelea kudokeza kuhusu ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni. Aprili 11 mashabiki wa mkali huyo walipagawa mara baada ya kuona mabango (Billboards) yenye ujumbe kuhusu album hiyo kwenye barabara za Jiji la California, Marekani. Hii itakuwa Album yake ya Nne ikiifuata ‘Astroworld’ ya mwaka 2018.

Read More
 KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Rapa Kanye West ameonesha mahaba kwa rafiki yake wa karibu kabisa Travis Scott, kwani ametishia ujiondoa kwenye tamasha la Coachella mpaka pale mwanamuziki mwenzake Billie Eilish atakapomuomba msamaha travis scott kwa kum-diss kwenye moja ya tamasha lake alilofanya wikendi iliyopita. Billie Eilish alim-diss Travis Scott kwenye tamasha lake akidai kuwa yeye huwa anasitisha show kama mashabiki wakiwa katika hali mbaya. Kauli ambayo ilitajwa kumlenga rapper Travis Scott ambaye aliripotiwa kushindwa kusitisha tamasha lake la Astro-World festival baada ya baadhi ya mashabiki kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya mwaka wa 2021. Hata hivyo Billie Eilish  ameibuka na kukanusha taarifa hizo kwa kusema kwamba hakuwa na nia ya kum-diss Travis Scott kama inavyotafsiriwa ila alikuwa anatoa msaada tu kwa shabiki.

Read More
 KAMPUNI YA DIOR WASITISHA MKATABA WAO NA RAPA TRAVIS SCOTT

KAMPUNI YA DIOR WASITISHA MKATABA WAO NA RAPA TRAVIS SCOTT

Kampuni ya Fashion ya Dior imeamua kusitisha mkataba wake na Rapa Travis Scott, mkataba uliokuwa uanze mwakani 2022 kutokana na kisa kilichomkuta msanii huyo katika tamasha lake la Astro world ambapo watu 10 walipoteza maisha. Kampuni hiyo imesema imefikia uamuzi huo kama heshima kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika Tamasha la Msanii huyo. Hivyo, hakutakuwa na ushirikiano tena kati ya Kampuni hio kubwa ya usambazaji wa mavazi na msanii huyo. Huu ni muendelezo wa matukio ya kupoteza mikataba mbalimbali kwa Travis Scott baada ya Kampuni ya Anheuser-Busch kusitisha usambazaji wa vinywaji vya Cacti ambavyo ni vinywaji vya Travis. Mbali na kupoteza mikataba, tayari mashtaka zaidi ya 100 yamefunguliwa dhidi ya msanii huyo kwa kufanya show isiyokuwa na tahadhari na hivyo kusababisha vifo vya watu.

Read More
 JINAMIZI LAZIDI KUMUANDAMA TRAVIS SCOTT,MSANII WAKE AAHIDI KUFUNGUKA MAZITO

JINAMIZI LAZIDI KUMUANDAMA TRAVIS SCOTT,MSANII WAKE AAHIDI KUFUNGUKA MAZITO

Misala haiishi kwa Travis Scott, mwaka wa 2021 unakuwa mwaka mbaya kwake. Baada ya msala wa Astroworld sasa ni zamu ya msanii wake mpya Malu Trevejo Msanii huyo wa kike wa Travis anamshinikiza Rapa huyo kumuachia ajitoe kwenye uongozi wake kabla hajaanza kutoa ma-file yake mabaya Malutrevejo ameandika jumbe mbalimbali kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram akimtaka rapa huyo kuvunja nae mkataba la sivyo ataanika madudu yote. Travis Scott alimsaini Malu Trevejo mapema mwaka huu baada ya kukiona kipaji chake kupitia mtandao wa TikTok. Miezi mitatu baadaye, Malu alitangaza kujitoa kwenye label hiyo (Cactus Jack) na Kutangaza kujiunga na Atlantic Records.

Read More
 TRAVIS SCOTT AONDOLEWA KWENYE ORODHA YA WATUMBUIZAJI WA TAMASHA LA COACHELLA 2022

TRAVIS SCOTT AONDOLEWA KWENYE ORODHA YA WATUMBUIZAJI WA TAMASHA LA COACHELLA 2022

Rapa kutoka nchini Marekani Travis Scott ameondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa tamasha la Coachella kwa mwaka 2022 kufuatia tukio la vifo vya watu 10 kwenye tamasha lake Astroworld Festival mwezi November mwaka huu. Hii imekuja mara baada ya watu kuleta mapingamizi mtandaoni wakitaka rapa huyo kuondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji, mapingamizi ambayo yalifikia saini 60,000. Ikumbukwe Tamasha la Astroworld Festival ambalo liliandaliwa na Travis Scott kwa lengo kusaidia elimu kwa vijana wadogo, lilikumbwa na simanzi mara baada ya watu takribani 11 kufariki dunia na wengine kujeruhiwa wakati onesho hilo likiendelea, hivyo kupelekea kuahirishwa.

Read More