Trey Songz Achunguzwa kwa Madai ya Kumshambulia Mpiga Picha New York
Msanii maarufu wa R&B, Trey Songz, anachunguzwa na polisi kwa madai ya kumshambulia mpiga picha kwenye mgahawa wa The Ivy mjini New York, tukio lililotokea Jumapili asubuhi. Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ, mpiga picha aitwaye Isaa Mansoor anadai kuwa alipewa kazi rasmi ya kurekodi matukio ya Trey Songz ikiwemo picha na video ndani ya mgahawa huo. Isaa anasema Trey alifahamu vyema kuwa kulikuwa na kamera mahali hapo, na kwamba kazi hiyo ilikuwa ya maandalizi. Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla baada ya mashabiki kuanza kumuomba Trey kupiga nao picha. Inadaiwa kwamba msanii huyo alionekana kukerwa na hali hiyo. Baadaye, wakati mmiliki wa mgahawa alipomwomba apige picha ya mwisho mbele ya nembo ya mgahawa huo, ndipo ghasia zilipozuka. Isaa anadai kuwa Trey alimchapa ngumi kichwani bila tahadhari, akamsukuma ukutani na kuvunja kamera zake mbili za kazi. Tukio hilo limewasilishwa kwa polisi wa New York na uchunguzi rasmi unaendelea. Hadi sasa, Trey Songz bado hajatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na madai haya.
Read More