Asili ya Trio Mio Yafichuliwa: Ni Mluya wa Kakamega

Asili ya Trio Mio Yafichuliwa: Ni Mluya wa Kakamega

Mama mzazi wa rapa chipukizi anayevuma nchini Kenya, Trio Mio, amefichua kwa mara ya kwanza kwamba mwanawe ni Mluya kutoka Kaunti ya Kakamega. Taarifa hiyo imeweka wazi mjadala wa muda mrefu kuhusu chimbuko la kijana huyo maarufu katika tasnia ya muziki. Kupitia Instagram live, mama yake Trio Mio alisema kuwa japo watu wengi walidhani mwanawe anatoka maeneo ya Pwani au Nairobi pekee, ukweli ni kuwa ana asili ya jamii ya Waluhya na hasa kutoka eneo la Kakamega. “Ni kweli, Trio Mio ni Mluya. Baba yake anatoka Kakamega, na tuna fahari kubwa na mizizi hiyo,” alisema mama huyo ambaye mara nyingi huonekana kumsaidia mwanawe katika safari yake ya muziki. Trio Mio, ambaye jina lake halisi ni TJ Mario Kasela, alizaliwa mnamo mwaka 2004 na alipata umaarufu kupitia vibao maarufu kama Cheza Kama Wewe na Vumilia. Uwezo wake wa kurap kwa lugha ya Kiswahili na Sheng’ umemfanya kuwa miongoni mwa wasanii wanaopendwa sana nchini Kenya, hasa miongoni mwa vijana. Kauli ya mama yake imepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya wameonesha furaha kubwa, wakimkaribisha msanii huyo kama mmoja wao. Wengine wamesema kuwa asili hiyo haijawahi kuwa wazi awali, hivyo taarifa hiyo imeongeza ukaribu na uelewa wa mashabiki kuhusu maisha ya binafsi ya rapa huyo. Mbali na kazi yake ya muziki, Trio Mio amekuwa akijulikana pia kwa ukaribu wake na familia, hasa mama yake ambaye ameendelea kumsaidia kusimamia maisha na taaluma yake tangu aanze kuvuma kimuziki.

Read More
 Mama mzazi wa msanii Trio Mio amkingia kifua kwa madai ya kufeli mtihani wa KCSE 2022

Mama mzazi wa msanii Trio Mio amkingia kifua kwa madai ya kufeli mtihani wa KCSE 2022

Mama mzazi wa msanii Trio Mio, Irma Sofia amepuzilia mbali madai yanayotembea mtandaoni kuwa mwanaye alipata alama ya D kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE. Kupitia mitandao yake kijamii mwanamama huyo amemkingia kifua mwanaye kwa kusema kuwa hitmaker huyo wa “Cheza Kama Wewe” alifanya vizuri kwenye mtihani huo na anajivunia matokeo yake. “Kooo Sasa Sitabreathe coz KCSE results zimetoka?? Tulieni. The boy did his best and am very proud of him. And those speculating a D ….poleni!”, Ujumbe wake ulisomeka. Mara tu baada ya waziri wa elimu Ezekiel Machogu kutangaza rasmi matokeo hayo, walimwengu kwenye mitandao ya kijamii waliibua madai kuwa Trio Mio alipata alama ya D kwenye mtihani wa KCSE 2022. Hata hivyo mpaka sasa hajabainika wazi msanii huyo amepata alama ipi kwenye wa ke wa KCSE ila baadhi ya wajuzi wa mambo mitandaoni wanadai kuwa alipata alama ya A-.

Read More
 Trio Mio afunguka kupotea kimuziki baada ya shule

Trio Mio afunguka kupotea kimuziki baada ya shule

Msanii Trio Mio amewajibu mashabiki zake ambao wanatilia shaka uwezo wake wa kuachia nyimbo kali baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne. Kwenye mahojiano na Vicent Mboya amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa shule ndio ilikuwa kizingiti kwenye suala la kuachia nyimbo mfululizo, hivyo anaamini kuwa kukamilisha kwake masomo kutamsaidia kuelekeza nguvu zake kuboresha muziki wake. Kauli yake imekuja baada ya walimwengu kuhoji kuwa huenda akakumbana na mambo yatakayomzuia kuendelea na muziki wake ikiwemo mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti.

Read More
 Trio Mio atoa ujumbe muhimu kwa familia na mashabiki katika siku yake ya kuzaliwa leo.

Trio Mio atoa ujumbe muhimu kwa familia na mashabiki katika siku yake ya kuzaliwa leo.

Rapa anayekuja kwa kasi nchini Trio Mio ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kufikisha umri miaka 18, Oktoba 22. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe mzito wa shukrani kwa familia, mashabiki na uongozi wake kwa kusimama naye kwenye safari yake ya muziki. “I’m officially legal! Just turned 18 today fam na naskia wah! Tuzidi kuzidi in this journey together. I thank God, my mama for giving birth to this fine pikin my sisters for always being there for me, my bro for being my shield, my team for the amazing work we do and you my fans for sticking with me through my growth as an artist. Kijana ako 18 na namada mesti Dec, mustake jua vile nakam na ubaya”, Ameandika. Hitmaker huyo wa “Cheza Kama Wewe” amesema zawadi kubwa ambayo mashabiki zake wanaweza kumpa kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake ni kuitazama video ya wimbo wake mpya uitwao “Hapa Kazi Tu.” inayopatikana kwenye mtandao wa Youtube. “Biggest gift mnaeza nipea ni kucheki ngoma yangu mbichi #HapaKaziTu. Like, comment, share & subscribe. Link kwa bio “, Ameongeza. Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali nchini akiwemo Nameless na Bien wa Sauti Sol wametakia msanii huyo salamu za heri kipindi hiki anasherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Utakumbuka Trio Mio kwa sasa anajianda kukalia mtihani wake wa kidato cha nne na juzi kati alitoa angalizo kwa wasanii wajipange kimuziki kwani atakaporejea kwenye tasnia ya muziki atawaonyesha kivumbi kwa kuachia nyimbo kali mfululizo bila kupoa.

Read More
 Trio Mio atangaza hali ya hatari kwa wasanii baada ya kuchukua mapumziko kwenye muziki

Trio Mio atangaza hali ya hatari kwa wasanii baada ya kuchukua mapumziko kwenye muziki

Rapa anayekuja kwa kasi nchini Trio Mio amechukua mapumziko mafupi kwenye muziki wake kwa ajili ya kujiandaa kukalia mtihani wake wa kitaifa wa kidato cha nne. Rapa huyo amethibitisha hilo kupita ukurasa wake wa twitter ambapo ametoa angalizo kwa wanamuziki wenzake kujipanga kisanaa la sivyo akirejea mwakani atawaonyesha kivumbi kwenye tasnia ya muziki. Hata hivyo kauli yake imezua hisia mseto miongoni mwa wakenya ambapo wengi wamemtaka rapa huyo aache majigambo na badala ya kuelekeza nguvu zake kwenye matayarisho ya mtihani wa kidato cha nne Utakumbuka Trio Mio ambaye ana umri wa miaka 18 alipata umaarufu nchini kipindi cha corona kupitia wimbo wake uitwao Cheza Kama Wewe na tangu kipindi hicho amekuwa akiachia nyimbo mfululizo bila kupoa kiasi cha watu kuanza kumfananisha na Marehemu E-Sir, moja kati ya marapa walioacha alama kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Kenya.

Read More
 TRIO MIO AKANUSHA KUPATA D+ KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KCSE

TRIO MIO AKANUSHA KUPATA D+ KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KCSE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya Trio Mio amekanusha tetesi zinazosambaa mtandaoni kuwa alipata alama D+ kwenye mtihani wa kitaifa wa KCSE wa mwaka wa 2021. Katika mahojiano ya hivi karibuni Trio Mio amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa bado anaendelea na masomo yake ya Shule ya upili. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Step” amepulizia mbali madai ya kusomea nyumbani kwa  kusema kwamba bado anasomea shule za bweni. Kauli yake imekuja mara baada ya watu kusambaza uvumi mtandaoni kuwa msanii huyo amepata alama ya D+  pindi tu waziri wa elimu Prof. George Magoha alipotangaza matokea ya mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka wa 2021

Read More
 TRIO MIO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA JUKWAA LA KUTOA MASOMO MTANDAONI DARASA AFRICA.

TRIO MIO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA JUKWAA LA KUTOA MASOMO MTANDAONI DARASA AFRICA.

Staa mpya wa muziki nchini Trio Mio ameingia ubia wa kufanya kazi na Darasa Afrika jukwaa la kutoa mafunzo kwa wanafunzi mtandaoni. Trio Mio ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Darasa Afrika. Hitmaker huyo wa “Steppa” amewataka wanafunzi walio kwenye likizo kuendeleza masomo yao mtandaoni kupitia jukwaa la Darasa Afrika wakati huu shule zimefungwa. Kwa sasa Trio Mio atatakiwa kutangaza huduma za Darassa Afrika kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongeza jukwaa hiyo wanafunzi watakaopata maarifa kupitia masomo wanayotoa kwa njia ya mtandao.

Read More
 SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

SSARU AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA TRIO MIO

Female rapper kutoka Kenya Sylvia Ssaru ameibuka na kukanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na msanii mwenzake Trio Mio. Hii ni baada ya wawili hao kuonekana kuwa na ukaribu katika siku za hivi karibuni toka walipoachia ngoma ya pamoja iitwao “Kichwa tu” ambayo wamemshirikisha Timmy Tdat. Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka kujua kama kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Trio Mio kwenye mtandao wa instagram Ssaru amesema hakuna kitu chochote kinaendelea kati yake na trio mio huku akidai kuwa uhusiano wao utabaki kuwa wa ndugu na dada. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumshambulia Ssaru ambapo wengi wamedai kuwa mrembo huyo ambaye ni mkubwa kiumri ana mpango wa kumharibu kimaadili Trio Mio ambaye bado anasoma shule ya upili.

Read More