Twitter yafanya mabadiliko katika sehemu ya search

Twitter yafanya mabadiliko katika sehemu ya search

Twitter imefanya mabadiliko katika sehemu ya search. Sasa hivi unaweza kuona thamani ya hisa na cryptos katika sehemu ya Search. Mfano ukitaka kutazama thamani ya hisa za Apple kwa sasa unaweza kuandika $aapl au $AAPL na utaona thamani ya hisa za Apple kwa ripoti ya siku. Inaonekana unaweka $ kama ukitaka kuona thamani ya hisa au crypto kwa Dola. Lakini ukiweka alama za ¥ € ¥ £ ₦ bado hauwezi kuona thamani ya hisa na crypto kwa currencies zaidi ya Dola. Kwa twitter ni idea nzuri kwa sababu mtandao huu unatumika sana na watu wengi kufuatilia trends za Hisa na Cryptocurrencies. Inaonekana imeshirikiana na Robinhood kuweka graphs na bei za hisa na crypto.

Read More
 Twitter rasmi yaondoa utambulisho wa vifaa vya simu kwa watumiaji wake

Twitter rasmi yaondoa utambulisho wa vifaa vya simu kwa watumiaji wake

Mtandao wa Twitter rasmi umeondoa utambulisho wa vifaa vya simu chini ya Tweet za watumiaji wake. Sasa hautaweza tena kuona (Tweet for iPhone au Tweet for Android) kwenye Tweets. Uamuzi huu umekuja mara baada ya mmiliki mpya Elon Musk kushika hatamu. Mwezi November mwaka huu Elon Musk alitangaza kuwa atafanya mabadiliko hayo kutokana na kuwa utambulisho huo unafinya nafasi “Waste of screen space” na hakuna anayefahamu sababu ya kwanini utambulisho huo uliwekwa.

Read More
 TWITTER KUWEKA SEHEMU YA KU-RETWEET KWA KUTUMIA PICHA NA VIDEO

TWITTER KUWEKA SEHEMU YA KU-RETWEET KWA KUTUMIA PICHA NA VIDEO

App ya Twitter inaongeza sehemu mpya katika option za ku-retweet ambayo itaitwa “Quote Tweet with reaction”. Sehemu hii itawezesha watumiaji kuonyesha reaction zao katika Tweet kwa kutumia video au picha. Mfano unaweza kuona tweet, ukaamua kupiga picha ya kureact (kujibu tweet au kuelezea tweet). Picha hiyo inaambatana na tweet ambayo “ume-retweet with reactions”. Ukipost zote zinakaa pamoja katika post moja – picha/video na tweet ambayo ume-retweet. Kwa Twitter hii inaweza kutumika vibaya hasa katika meme au social trends kwa sababu watu wanaweza kufanya jokes katika tweets za watu.

Read More
 TWITTER KUWEKA MATANGAZO KATIKA SEHEMU YA REPLIES

TWITTER KUWEKA MATANGAZO KATIKA SEHEMU YA REPLIES

Mtandao wa Twitter umeanza majaribio ya kuweka matangazo katika sehemu ya Replies/comments. Ni style mpya ya kuonyesha matangazo katikati ya comments/replies. Inaonekana matangazo yataonekana sana katika Tweets za watu maarufu na akaunti ambazo zina watu wengi wanaoshiriki katika comments. Bado haijaonekana kama mwenye akaunti atafaidika na matangazo ambayo yataonekana katika Replies za Tweets zake. Tayari imeanza kwa watumiaji wa App ya Beta katika iOS na Android.

Read More