TYGA NA ROB KARDASHIAN WAMCHANA BLAC CHYNA BAADA YA KUSEMA HAPEWI PESA ZA MATUNZO YA WATOTO
Rapa kutoka Marekani Tyga pamoja na Rob Kardashian wameamua kwa pamoja kumtolea uvivu Blac Chyna ambaye ni mama wa watoto wao baada ya kusema hadharani kwamba hapewi pesa za matunzo ya watoto na ameamua kuuza magari yake matatu kwa ajili ya kupata pesa za kujikimu. Tyga ambaye ana mtoto mmoja na Chyna (King Cairo Stevenson) alikuwa wa kwanza kuibuka kwenye comment katika post hiyo ya Blac Chyna ambayo imepostiwa kwenye ukurasa wa The Shaderoom Instagram, kwa kuandika ujumbe unaosomeka “Nalipa ($40K) zaidi ya shilling million 4.6 kwa mwaka kwa ajili ya Ada ya mtoto wangu shule, na ninaishi naye toka Jumatatu hadi Jumamosi. Kwanini nilipe pesa za matunzo ya mtoto.” aliandika Tyga na kumalizia kwa kicheko. Rob Kardashian ambaye pia wamezaa mtoto mmoja (Dream Renèe Kardashian) alikuja na kuacha comment yake isemayo “Nalipa ($37k) zaidi ya shilling million 4.3 za Kenya kwa mwaka kama Ada ya shule ya binti yangu. Ninasimamia gharama zote za matibabu. Nalipa gharama zote za ziada kwa binti yangu. Ninakuwa naye kuanzia Jumanne hadi Jumamosi. Kwanini nilipe pesa ya matunzo ya mtoto.” aliandika Rob Kardashian.
Read More