Kenya Kuandaa Fainali za CHAN 2025 Kasarani

Kenya Kuandaa Fainali za CHAN 2025 Kasarani

Kenya imepata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali ya makala ya nane ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN), itakayochezwa tarehe 30 Agosti 2025 katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi, Kasarani. Hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kuwa mwenyeji wa fainali ya mashindano haya ya kipekee barani Afrika. Mashindano hayo yataandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kenya, Tanzania na Uganda. Mechi ya ufunguzi itachezwa Dar es Salaam tarehe 2 Agosti, mechi ya nafasi ya tatu Kampala, na fainali kufanyika jijini Nairobi. Kenya itaongoza Kundi A litakalojumuisha Morocco, Angola, DR Congo na Zambia. Uwanja wa Kasarani unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kufanikisha maandalizi ya fainali hiyo, ikiwemo maboresho ya taa, mfumo wa VAR, na huduma za mashabiki. Serikali kwa kushirikiana na FKF imeahidi kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa viwango vya kimataifa. Mashindano ya CHAN yanatoa jukwaa la kuibua vipaji vya wachezaji wa ndani, huku pia yakitarajiwa kuongeza mapato kupitia utalii na biashara. CAF inatarajiwa kutangaza ratiba kamili ya mechi na taratibu za tiketi hivi karibuni.

Read More
 Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza nia yake ya dhati ya kushirikiana na msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, katika wimbo mpya unaotarajiwa kutoka mwaka huu. Akiwa jukwaani katika tamasha la Coffee Marathon huko Ntungamo, Uganda, Diamond aliwajulisha mashabiki kuwa kolabo hiyo ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu, na sasa anafanya kila juhudi kuhakikisha inatimia. Diamond alisema kuwa licha ya mafanikio yake makubwa katika bara la Afrika, hajawahi kusahau mchango wa Jose Chameleone katika muziki wa Afrika Mashariki. Alimuelezea kama msanii aliyeathiri kizazi kizima na kumvutia hata yeye kuingia kwenye tasnia ya muziki. “Mwaka huu nataka kuhakikisha ninafanya wimbo na Jose Chameleone. Tunamshukuru Mungu kuwa anaendelea vizuri kiafya na tunamshukuru kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki,” alisema Diamond mbele ya mashabiki. Kwa upande wake, Jose Chameleone, ambaye ametamba kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki kuwa moja ya nguzo za muziki wa Afrika Mashariki, bado anaheshimika kwa nyimbo zake zenye ujumbe mzito na sauti ya kipekee. Kolabo kati ya Chameleone na Diamond inatarajiwa kuwa ya kihistoria, na tayari mashabiki kote kanda ya Afrika Mashariki wanasubiri kwa hamu kusikia kazi yao ya pamoja.

Read More
 Catherine Kusasira Atishia Kujiondoa NRM Kufuatia Kudharauliwa na Viongozi wa Chama

Catherine Kusasira Atishia Kujiondoa NRM Kufuatia Kudharauliwa na Viongozi wa Chama

Msanii na mshauri wa Rais wa Uganda kuhusu masuala ya Kampala na wakazi wa Ghetto, Catherine Kusasira, ametishia kujiondoa ndani ya chama tawala cha NRM, akilalamikia kile alichokiita dharau na kutotambuliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho. Kusasira amesema licha ya kujitolea kwa miaka karibu kumi kutetea chama na Rais Yoweri Kaguta Museveni, bado anakumbana na vikwazo na kudharauliwa, hasa na maafisa wa usalama na baadhi ya viongozi waandamizi wa NRM. “Nimechoka na dharau kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya NRM. Mnathubutu kunizuia kukutana na Jenerali Nalweyiso? Nimejitolea kwa ajili ya chama, lakini ni Rais pekee anayetambua juhudi zangu. Wakati mwingine nawaza kuacha siasa kabisa,” alisema Kusasira. Msanii huyo ambaye hapo awali alitangaza nia ya kugombea kiti cha Mwakilishi wa Wanawake wa Buikwe, anaonekana kupoa kisiasa na sasa anaelekeza nguvu zake katika kukuza chama kwa njia ya ushawishi na kampeni za kijamii. Kwa sasa, Kusasira anasisitiza kuwa mchango wake unapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa na viongozi wote wa chama, sio Rais peke yake. Kauli yake imezua mijadala mikali ndani ya chama, huku wachambuzi wa siasa wakitathmini athari za manung’uniko yake kwa taswira ya NRM miongoni mwa wasanii na vijana

Read More
 Cindy Sanyu Asema Hakujua Kuhusu Tamasha la Dax Vibes, Amshauri Aahirishe Kama Ana Hofu

Cindy Sanyu Asema Hakujua Kuhusu Tamasha la Dax Vibes, Amshauri Aahirishe Kama Ana Hofu

Msanii maarufu wa Uganda, Cindy Sanyu, ametoa ufafanuzi kuhusu mgongano wa tarehe za matamasha kati yake na Dax Vibes, akieleza kuwa hakujua kuhusu tamasha lake hadi baada ya kutangaza tarehe ya onyesho lake mwenyewe. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Cindy amesema hakuwa na nia ya makusudi kupanga tamasha lake siku hiyo, lakini anashauri Dax kuahirisha endapo anaona kushiriki tarehe hiyo ni changamoto.  “Sikujua kuhusu tamasha lake hadi nilipotangaza tarehe yangu. Kama anaogopa kushiriki tarehe hiyo na mimi, anaweza kuahirisha. Si jambo la ushindani,” alisema Cindy. Akiweka wazi uzito wa tukio hilo, Cindy alifichua kuwa tarehe 28 Agosti ina maana kubwa sana kwake kwani si tu siku ya kuzaliwa kwake kwa mara ya 40, bali pia inaadhimisha miaka 26 ya safari yake ya muziki. “Siku hiyo ni ya kihistoria kwangu – ni birthday yangu ya miaka 40 na miaka 26 kwenye muziki. Ni tamasha lenye maana ya kibinafsi sana,” aliongeza. Tofauti hiyo ya tarehe imesababisha gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakitoa maoni tofauti. Wengi wamesimama na Cindy kwa msingi wa muda aliokaa kwenye tasnia ya muziki na alama ya mafanikio anayosherehekea. Wengine pia wanatoa wito kwa wasanii hao wawili kuonyesha mshikamano na kusaidiana badala ya kushindana. Kwa sasa, mashabiki wanaendelea kusubiri kuona iwapo Dax Vibes atazingatia ushauri huo au ataendelea na mpango wake wa tamasha katika tarehe ileile.

Read More
 Azawi Afichua Kuwekeza Milioni 24 Kurekebisha Meno

Azawi Afichua Kuwekeza Milioni 24 Kurekebisha Meno

Mwanamuziki wa Uganda, Azawi , amefunguka kuhusu uwekezaji mkubwa alioufanya kuboresha tabasamu lake, baada ya kupata mafanikio makubwa chini ya lebo ya Swangz Avenue. Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji wa YouTube, Kasuku, Azawi alieleza kuwa alitumia kiasi cha shilingi milioni 24 za Uganda (UGX) kurekebisha tatizo la meno lililosababishwa na ajali aliyopata alipokuwa katika umri mdogo. Msanii huyo alisema alianguka na kuvunjika taya, hali iliyosababisha mapengo yaliyoathiri muonekano wake kwa muda mrefu.  “Sikuwa na uwezo wa kuyarekebisha zamani, lakini baada ya kupata mafanikio kupitia muziki wangu chini ya Swangz Avenue, niliamua kuweka hilo suala sawa. Ilikuwa ni hatua ya binafsi na ya muhimu kwangu,” alisema Azawi. Katika mahojiano hayo, Azawi pia aligusia maisha yake ya kimapenzi, akifichua kuwa awali alikuwa katika mahusiano ya muda mfupi, lakini sasa yuko tayari kutulia. Kwa utani, alieleza kuwa hupendelea wanaume warefu na wanene, akisema haavutiiwi na wanaume wenye misuli (six-packs). Azawi anaendelea kung’ara katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki, na sasa si tu kwa sauti yake ya kipekee, bali pia kwa tabasamu linaloendana na jina lake kubwa. Swangz Avenue ilimsaini Azawi mwaka 2019 na kumtambulisha rasmi kwa umma tarehe 31 Oktoba mwaka huo. Tangu wakati huo, amejizolea umaarufu kwa nyimbo kama ‘Lo Fit’, ‘Masavu’, ‘Party Mood’, ‘Majje’, ‘Quinamino’, na ‘Ku Sure’.

Read More
 Fik Fameica: Pallaso Ni Shabiki Tu, Si Mlezi Wangu Kimuziki

Fik Fameica: Pallaso Ni Shabiki Tu, Si Mlezi Wangu Kimuziki

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Fik Fameica amevunja ukimya na kukanusha vikali madai ya msanii mwenzake Pallaso, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akidai kuwa alihusika pakubwa katika kukuza safari yake ya muziki. Hii ni baada ya Pallaso kudai kuwa alimtoa Fik Fameica kwenye mitaa ya Kawempe, na kumtambulisha kwenye muziki, na hata kumsaidia kifedha alipokuwa anaanza safari yake ya muziki. Hata hivyo, Fik Fameica kwenye mahojiano yake hivi karibuni ameyakana madai hayo akisema kwamba Pallaso hajawahi kutoa mchango wowote wa maana katika mafanikio yake. Alieleza kuwa Pallaso alikuwa tu shabiki kama walivyo mashabiki wake wengine. “Pallaso aliwadanganya. Hajawahi changia chochote katika safari yangu ya muziki. Alikuwa tu shabiki wangu, si zaidi ya hapo,” alisema Fameica katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Fameica alisisitiza kuwa yeye ni msanii aliyejijenga mwenyewe (self-made), na kwamba mafanikio yake yalianza mara ya kwanza tu alipoingia studio. “Mimi ni msanii aliyejijenga. Mara ya kwanza niliingia studio, nilitoa kibao ‘Pistol’ ambacho kilipokelewa vizuri,” aliongeza. Fik Fameica alipata umaarufu mkubwa mwaka 2018 kupitia wimbo wake maarufu “Kutama”, na tangu wakati huo amekuwa akitoa nyimbo kali mfululizo na kumuweka katika nafasi ya juu kama mmoja wa wasanii bora zaidi katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki.

Read More
 Azawi Kutumia Muziki Kupaza Sauti za Waganda Walionyimwa Haki

Azawi Kutumia Muziki Kupaza Sauti za Waganda Walionyimwa Haki

Mwanamuziki wa Uganda, Priscilla Zawedde maarufu kama Azawi, ameweka wazi dhamira yake ya kutumia muziki kama chombo cha kupaza sauti dhidi ya dhuluma na ukosefu wa haki nchini mwake. Hii ni baada ya takriban miaka miwili ya kuikosoa serikali hadharani kupitia majukwaa mbalimbali. Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Uganda, Azawi alieleza kuwa yupo mbioni kuingia studio kurekodi nyimbo za mapinduzi zenye ujumbe mzito unaoelezea machungu na hali halisi ya wananchi wa kawaida. “Nataka kuonesha maumivu ya Waganda wengi kupitia muziki wangu,” alisema Azawi. “Nafanya kazi juu ya hilo, na label yangu Swangz Avenue wanaheshimu maoni na mtazamo wangu.” Akiwa chini ya usimamizi wa lebo ya Swangz Avenue, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Talking Stage” alisisitiza kuwa hana hofu ya kupoteza nafasi yake kwenye lebo hiyo, endapo msimamo wake wa kisanii hautaungwa mkono. “Ikiwa hawatataka kufanya kazi nami kwa sababu ya nyimbo hizo, ni sawa tu. Nitajiondoa,” alisema kwa msimamo thabiti. Azawi anaelekea kufungua ukurasa mpya wa muziki wenye uzito wa kijamii na kisiasa, hatua ambayo huenda ikamuweka kwenye mgongano na serikali au hata wasimamizi wake wa kazi za usanii lakini pia inaweza kumweka katika nafasi ya kipekee kama msanii anayesimama kwa ajili ya watu wake. Hata hivyo mashabiki wake wameonyesha msisimko mkubwa mtandaoni, wakimpongeza kwa ujasiri na nia ya kutumia muziki kama silaha ya kupigania haki na kuunganisha jamii.

Read More
 Nina Roz Afichua Sababu za Kujiondoa UNMF, Amsuta Vikali Eddy Kenzo kwa Kuwa Mbinafsi

Nina Roz Afichua Sababu za Kujiondoa UNMF, Amsuta Vikali Eddy Kenzo kwa Kuwa Mbinafsi

Mwanamuziki maarufu na mwanasiasa chipukizi, Nina Roz, ameibua mjadala mpya katika tasnia ya muziki nchini Uganda baada ya kufichua sababu zilizomfanya kujiondoa kwenye Shirikisho la Kitaifa la Wanamuziki nchini humo (UNMF) Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na vyombo vya habari, Nina Roz alieleza kuwa walibuni shirikisho hilo pamoja na  Eddy Kenzo kwa madhumuni ya kuwatetea wasanii, kusimamia haki zao, na kuendeleza ustawi wa sekta ya muziki nchini Uganda. Hata hivyo, alidai kuwa hali hiyo ilianza kubadilika muda mfupi baada ya kuanzishwa kwa shirikisho hilo mwaka 2023.  “Nilidhani tunaunda jukwaa la kweli la kuwaunganisha wasanii na kuwatetea, lakini baadaye nikabaini kuwa viongozi, hususan Eddy Kenzo, walikuwa na maslahi binafsi pamoja na ajenda za kisiasa ambazo hazikuwiana na malengo ya awali,” alisema Nina Roz. Nina, ambaye aliwahi kushika wadhifa wa kusimamia masuala ya maadili ndani ya UNMF, alieleza kuwa shirikisho hilo lilianza kupoteza dira na kuonyesha ukaribu usiofaa na serikali. Kwa maoni yake, hali hiyo ilikuwa kinyume na misingi ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa kisanii. Tangu kujiondoa kwake, Nina Roz amekuwa mkosoaji wa wazi wa shirikisho hilo, akilituhumu kwa kile alichokitaja kuwa ni siasa za upendeleo katika tasnia ya muziki. Anadai kuwa wasanii wanaoonekana kukosoa serikali wamekuwa wakibaguliwa katika upatikanaji wa fursa, mikataba, na msaada kutoka kwa taasisi hiyo. “UNMF haikuwakilisha tena maslahi ya wasanii wote. Iligeuka kuwa jukwaa la upande mmoja, ambapo wale waliokuwa karibu na serikali ndio walipewa kipaumbele,” aliongeza. Kwa sasa, Nina Roz anajiunga na orodha ya wasanii wakubwa kama King Saha, Ziza Bafana, na Spice Diana, ambao wote wamejitenga na UNMF, wakieleza kutoridhishwa  na namna taasisi hiyo inaendeshwa.

Read More
 Pallaso Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Siasa

Pallaso Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Siasa

Msanii maarufu wa muziki nchini Uganda, Pius Mayanja almaarufu Pallaso, amesema kwa sasa hana mpango wa kujiingiza kwenye masuala ya siasa, akisisitiza kuwa bado anajikita kikamilifu katika taaluma yake ya muziki. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Pallaso alieleza kuwa hajatimiza malengo aliyojiwekea katika muziki, na hivyo anataka kuyakamilisha kabla ya kufikiria kuchukua jukumu lolote jipya katika maisha yake ya kitaaluma.  “Sihitaji kuingia kwenye siasa kwa sasa. Niko katika harakati za kutimiza ndoto yangu ya muziki, na nataka kuikamilisha kikamilifu kabla ya kufikiria jambo lolote jingine.” Ingawa hajajitosa rasmi katika siasa, Pallaso alisema anaendelea kutumia muziki wake kama chombo cha kuwasilisha ujumbe wa kijamii na kisiasa. Anaamini kuwa muziki ni jukwaa lenye nguvu kubwa la kufikisha ujumbe, na ndilo eneo analolielewa vyema. “Siasa ni wito. Binafsi bado sijaupata. Nikihisi moyoni kwamba ni wakati wa kuingia katika siasa, nitafanya hivyo. Lakini kwa sasa, ninaendelea kuwasilisha ujumbe wangu kupitia muziki.” Kauli ya Pallaso inajiri wakati ambapo baadhi ya wasanii nchini Uganda wameanza kujitosa katika siasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Miongoni mwao ni Big Eye na Nina Roz, ambao tayari wametangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa. Ingawa Pallaso hana pingamizi kwa wasanii kuingia katika siasa, amesema ataingia katika ulingo huo pale tu atakapohisi kwa dhati kuwa ni wito wake wa kweli kulitumikia taifa. Kwa sasa, anabaki kuwa mmoja wa wasanii wanaotumia kazi zao kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Read More
 “Warembo Wanapenda Mali, Sio Ndoa” – Msanii Chris Evans

“Warembo Wanapenda Mali, Sio Ndoa” – Msanii Chris Evans

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Chris Evans, ametangaza rasmi kuachana na wanawake warembo, akisema hawana nia ya dhati ya kuingia kwenye ndoa. Evans, ambaye amewahi kuhusishwa kimapenzi na mastaa kama Zanie Brown, Spice Diana, na Lydia Jazmine, amesema kwamba wanawake wengi warembo huwa wanavutiwa na mali na si kujenga familia. Mwanamuziki huyo anayefahamika kwa kibao chake maarufu “Linda”, amesema kwa sasa moyo wake umeelekezwa kwa wanawake wa muonekano wa wastani, ambao kwa mtazamo wake wana sifa ya unyenyekevu, uaminifu, na nia ya kweli ya kuanzisha ndoa ya kudumu. “Nimeacha kuwahangaikia wanawake warembo kwa sababu hawana nia ya kweli. Wengi wao wanawinda pesa na hata hawafai kwa ndoa. Nitawachagua wale walio na mwonekano wa wastani kwa sababu huwa ni uaminifu na wako tayari kuanzisha maisha ya ndoa,” alieleza. Chris Evans amesisitiza kuwa yuko tayari kutulia na mwanamke mmoja na kuanzisha familia yenye misingi imara ya upendo na uaminifu Hatua hii inaonekana kuwa mwanzo mpya kwa msanii huyo mkongwe, ambaye kwa muda mrefu ameonekana kwenye vichwa vya habari kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi na mastaa wa tasnia ya burudani nchini Uganda.

Read More
 GRENADE AFUNGUKA SABABU ZA WAREMBO WA UGANDA KUMGANDA KAMA GUNDI

GRENADE AFUNGUKA SABABU ZA WAREMBO WA UGANDA KUMGANDA KAMA GUNDI

Msanii kutoka nchini Uganda Grenade amefunguka siri ambayo imewafanya wanawake wengi nchini humo kumpenda bila sababu za msingi. Kwenye mahojiano na Galaxy FM Grenade amejitapa kuwa ana ujuzi wa kipekee linapokuja swala la kutumia ulimi wake kuwashawishi wanawake ambapo ameenda mbali zaidi na kujinasibu kuwa swala hilo limewafanya wanawake wengi nchini uganda kumzimia kimapenzi. Grenade amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na wanawake wengi nchini uganda akiwemo  Lydia Jazmine, Vivian Mbuga, Sheila Gashumba, Zari na wengine wengi. Hata hivyo mbinu anazozitumia  Grenade kuwavutia warembo hao limeilkuwa kitendawili kwa  waganda wengi lakini Good news kuwa msanii huyo amenyoosha maelezo kuhusu hilo

Read More