Malipo ya Diamond Yatikisa Uganda, Wasanii Aibua Mjadala Moto

Malipo ya Diamond Yatikisa Uganda, Wasanii Aibua Mjadala Moto

Msanii mashuhuri wa Uganda, Allan Toniks, amezua gumzo mitandaoni baada ya kulalamikia hadharani kiwango kidogo cha malipo alichopewa kwa kushiriki tamasha moja nchini humo. Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Toniks alifunguka kwa hasira kwamba alipewa chini ya dola 1,000, huku akishangaa serikali ya Uganda kutumia shilingi milioni 750 kumlipa staa wa Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushiriki kampeni ya kuhamasisha kahawa. “Na wanakuja kunipa chini ya dola 1000, nikikataa wanasema najifanya. 750M UGX? Acheni ujinga.” Aliandika kwa hasira. Kauli ya Toniks ilisambaa kwa kasi, ikizua mjadala mkubwa. Baadhi ya watu walimtetea, wakisema ni wazi kuwa wasanii wa ndani wanadharauliwa na kutopewa thamani stahiki licha ya mchango wao katika kukuza utamaduni wa nchi. Wengine walidai kuwa fedha hizo zingeweza kusaidia miradi ya kijamii au kuimarisha sanaa ya ndani, wakikumbusha kuwa wakazi wa Kiteezi wanahitaji milioni 200 pekee kuboresha maisha yao. Hata hivyo, wapo waliotetea hatua ya kumleta Diamond, wakisema ni msanii mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika na kwamba uwepo wake unaleta mvuto wa kimataifa kwa kampeni ya kahawa. Kwao, hii ni mbinu ya kibiashara na kimkakati ambayo inaweza kusaidia sekta ya kilimo kuvuka mipaka. Tukio hili limeibua maswali kuhusu vipaumbele vya serikali ya Uganda, thamani ya sanaa ya ndani, na nafasi ya wasanii katika miradi ya kitaifa. Pia limeibua changamoto kwa wasanii wa Uganda kuwekeza zaidi katika kuboresha nembo zao binafsi ili kujiongezea heshima na nafasi kwenye majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Read More
 Eddy Kenzo Kutatua Mgogoro wa Ofisi za UMA Zilizofungwa kwa Madeni

Eddy Kenzo Kutatua Mgogoro wa Ofisi za UMA Zilizofungwa kwa Madeni

Rais wa Shirikisho la Wanamuziki Uganda (UNMF) na mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Uganda katika masuala ya ubunifu, Eddy Kenzo, ameahidi kuingilia kati na kusaidia Chama cha Wanamuziki Uganda (UMA) kurejeshewa ofisi zake zilizofungwa kutokana na deni la kodi. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini humo, Kenzo amesema hatua hiyo inalenga kutunza heshima ya taasisi ya UMA ambayo, kwa mujibu wake, imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya muziki nchini Uganda kabla ya kuanzishwa kwa UNMF. “Hatuwezi kuwaacha katika hali hii. UMA walifanya kazi kubwa kabla sisi hatujaja. Tutaingilia kati na kuona namna ya kuhakikisha ofisi zao zinafunguliwa tena,” alisema Kenzo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ndani. Kauli yake imekuja kufuatia hatua ya Kituo cha Kitaifa cha Utamaduni cha Uganda (UNCC), kinachomiliki jengo la National Theatre, kufunga rasmi ofisi za UMA kwa kile kilichoelezwa kuwa malimbikizo ya kodi ya karibu mwaka mmoja. Hatua hiyo imeathiri moja kwa moja uendeshaji wa shughuli za chama, huku ofisi za viongozi wakuu kama Cindy Sanyu (Rais wa UMA) na Phina Masanyalaze (Katibu Mkuu) zikiwa zimefungwa na kuwekewa zuio la kuingia. UMA, chini ya Cindy, imekuwa ikikosoa waziwazi uongozi wa UNMF na haswa Kenzo, huku mvutano kati yao ukijidhihirisha mara kadhaa katika majukwaa ya umma. Hata hivyo, Kenzo amechukua hatua ya kukutana na viongozi husika ili kushughulikia suala hilo kwa njia ya amani, akisema huu si wakati wa kutazama tofauti bali kushikamana kwa maslahi ya wanamuziki wote nchini Uganda. Sakata hili linaendelea kuwavutia wadau wengi wa sekta ya burudani nchini Uganda, huku wengi wakisubiri kuona ikiwa hatua ya Kenzo itazaa matunda na kumaliza mgogoro unaoathiri ustawi wa chama kongwe cha wanamuziki nchini.

Read More
 UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA UMA KUFANYWA JUNI 28

UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA UMA KUFANYWA JUNI 28

Hatimaye Chama cha Wanamuziki Uganda UMA imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho baada ya kufutwa kwa upigaji kura Juni 6 mwaka huu kutokana na kukumbwa na dosari. Katika mkao na wanahabari uma imesema uchaguzi huo utafanyika Juni 28 mwaka huu huko National Theatre garden jijini Kampala ambapo itafanyika kwa mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye kituo cha kupigia kura. Kulingana na uma upigaji wa kura katika chama hicho utafanyika  kwenye kituo kimoja hivyo wanachama wake watalazimika kusafari hadi kampala kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo kwani hawana pesa za kutosha kuandaa uchaguzi katika vituo vingi. Utakumbuka Uchaguzi wa UMA uliahirisha Juni 6 mara baada ya wafuasi wa King Saha kudai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi hadi sasa Kamati ya inayojishughulisha na uchaguzi hajatoa mweelekeo kama uchaguzi utarudiwa ila jambo la kusubiriwa.

Read More
 UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA WAAHIRISHWA

UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA WAAHIRISHWA

Kamati inayojishughulisha na uchaguzi katika Chama cha Wanamuziki nchini Uganda imeridhia ombi la msanii King Saha kuahirisha uchaguzi wa chama hicho ambao ungefanyika Mei 23 mwaka huu. Kupitia barua iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya chama cha UMA, uchaguzi wa chama hicho umeahirishwa kwa wiki mbili zaidi kutoa nafasi kwa tume ya uchaguzi kuboresha mifumo ya kupigia kura. Lakini pia kutoa elimu kwa wagombea wa wadhfa wa urais katika chama cha UMA kuhusu mbinu ambayo itatumika kuandaa uchaguzi wa chama hicho. Hata hivyo duru zimesema kwamba uchaguzi wa UMA umeahirishwa kutokana na shinikizo kutoka kwa umma baada ya watu kutilia shaka mchakato wa upigaji kura kwa njia ya sms ambao ungefanya uchaguzi huo kutokuwa wa haki na huru. Utakumbuka King Saha anachuana na mwimbaji mwenzake Cindy Sanyu kuwania urais wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda.

Read More
 CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI

CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI

Tume ya uchaguzi katika Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA) hatimaye, imetangaza tarehe mpya ambayo uychaguzi sambamba na mdahalo wa wagombea wa urais katika chama hicho utafanyika. Hapo awali, mdahalo huo ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu lakini haukufanyika kwa sababu zilizokuwa nje ya tume hiyo. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi katika chama cha UMA Bwana. Jeff Geoffrey Ekongot ameeleza kuwa mjadala huo utafanyika Mei 21 kabla ya zoezi la upigaji wa kura kung’oa nanga Mei 23 mwaka huu. Uongozi wa chama cha UMA hata hivyo umeshindwa kufafanua ikiwa upigaji kura katika chama hicho utafanyika kwa njia ya kidijitali, au kwa mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura. Utakumbuka wasanii King Saha na Cindy Sanyu wanatarajiwa kumenyana kwenye kinyang’anyiro cha urais katika chama cha uma ambapo mshindi katika uchaguzi huo ataongoza chama hicho kwa miaka miwili na nusu.

Read More