KAMPUNI YA UNIVERSAL MUSIC GROUP YAINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA THE WEEKND
Kampuni ya Universal Music Group imetangaza dili lake la ushirikiano na Mwanamuziki kutoka Marekani The Weeknd. Dili hilo linahusisha usimamizi wa kurekodi kazi zake, uchapishaji bidhaa na masuala ya video. Makubaliano hayo hayataathiri uhusiano wa The Weeknd na kampuni ya ‘UMG’s Republic Records’ ambayo ndiyo kampuni na mshirika wake wa muda mrefu katika kazi zake haswa za muziki tangu mwaka 2012. Hata hivyo kampuni ya UMG inayosimamia chapa (brand) na bidhaa za rappa huyo, itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Weeknd na XO ili kupanua na kuendeleza biashara ya kimataifa, biashara ya mtandaoni na fursa za leseni za rejareja kuhusu miradi na matoleo yajayo.
Read More