MENEJA VAGA AMKINGIA KIFUA STIVO SIMPLE BOY KWA TUHUMA ZA WIZI
Meneja wa Stivo Simple Boy Vaga amevunja kimya chake kuhusu tuhuma zilizotembea mtandaoni kuwa msanii wake alimuiba mpenzi wa mtu. Katika mahojiano yake na Captain Nyota vaga amesema madai ya Stivo kumchukua mpenzi wa mtu hayana ukweli wowote bali yanatumiwa na baadhi ya watu mtandaoni  kama daraja la kupata umaarufu kwenye vyombo vya habari nchini. Aidha amesema Stivo alimpata mpenzi wake kwa njia ya halali huku akisema msaniii huyo yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake ikiwa ni siku chache zimepita tangu wavishane pete ya uchumba. Kauli ya Vaga imekuja mara baada ya wanaume wawili kujitokeza kwenye nyakati tofauti na kudai kuwa stivo aliwaibia mpenzi wao kitu ambacho ambacho stivo mwenyewe alikanusha vikali mapema wiki hii.
Read More