VDJ Jones akanusha kuwakandamiza wasanii wa Jeshi Jinga

VDJ Jones akanusha kuwakandamiza wasanii wa Jeshi Jinga

Bosi wa lebo ya muziki ya Superstar Entertainment VDJ Jones amefunguka kuhusu madai ya kuvunja kundi la muziki wa Gengtone Jeshi Jinga. Kwenye mahojiano na Nicholas Kioko amesema madai ya kuinyanyasa kundi hilo kifedha hayana ukweli wowote huku akisema kuwa wasanii wa Jeshi Jinga wenyewe walishindwa kuachia muziki muzuri licha ya kutumia nguvu nyingi kuwatoa kisanaa. VDJ Jones amesema hajutii suala la kusitisha mkataba wa kufanya kazi na wasanii wa kundi hilo kwani walifeli kurudisha shillingi milioni mbili alizowekeza kwenye muziki wao. Sanjari na hilo amemkingia kifua mchekeshaji Eric Omondi kwa kusema kuwa mchekeshaji huyo anaiwazia mazuri tasnia ya muziki nchini Kenya ila wasanii wamefeli kumuunga mkono kwenye harakati za kuleta mabadiliko. Hata hivyo amewataka wasanii wa Kenya waache masuala ya kujihusisha sana na matukio yasiyokuwa na tija kwenye mitandao ya kijamii badala yake waachie nyimbo kali kama namna ambavyo wasanii wa Nigeria na Tanzania wanavyofanya.

Read More
 VDJ Jones akiri uhaba wa nyimbo mpya kwenye soko la muziki nchini Kenya

VDJ Jones akiri uhaba wa nyimbo mpya kwenye soko la muziki nchini Kenya

Bosi wa lebo ya Superstar Entertainment VDJ Jones amesikitishwa na maendeleo ya tasnia ya muziki nchini Kenya kwa kusema kwamba kuna uhaba mkubwa wa nyimbo mpya sokoni. Kupitia video aliyochapisha kwenye mtavndao Facebook VDJ Jones amesema kwa sasa madeejay wanapata ugumu wa kucheza muziki wa Kenya kwa kuwa wasanii hawatoi nyimbo kama kipindi cha nyuma, jambo ambalo liwamepelekea kuwategemea wasanii wa nje ambao wamekuwa wakiachia nyimbo mpya kila mara. Aidha amesema wasanii wa Kenya wasipotia bidii kwenye kazi zao za muziki huenda wasanii wa mataifa mengine wakateka soko la muziki nchini kwa  kutumbuiza kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Hata hivyo  ametoa changamoto kwa wasanii wa kenya kuanza kurekodi nyimbo mfululizo bila kupoa badala ya kusubiri wawe vizuri kiuchumi ndio waachie audio pamoja na video kwani mashabiki hawana subira. Kauli ya VDJ Jones inakuja wakati huu mchekeshaji Eric Omondi anaendelea kuwashinikiza wasaniii waachie nyimbo kwa kuwa wabunifu kwenye suala la kutengeneza matukio yatakayowafanya wazumngumzie kwenye vyombo vya habari.

Read More
 VDJ JONES AJIBU TUHUMA ZA KUWAIBIWA WASANII ZILIZOIBULIWA NA MSANII PARROTY

VDJ JONES AJIBU TUHUMA ZA KUWAIBIWA WASANII ZILIZOIBULIWA NA MSANII PARROTY

Dj maarufu nchini Vdj Jones amenyosha maelezo kuhusu madai yaliyoibuliwa na Parroty kuwa hajawahi walipa wasanii aliowashirikisha kwenye project zake.. Katika mahojiano na Plug tv Vdj Jones amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa amekuwa akiwalipa wasanii wote aliowashikisha kwenye kazi zake kwa usawa DJ huyo ameenda mbli zaidi na kusema kwamba ameshangazwa na msanii huyo kumuongelea vibaya mtandaoni ikizingatiwa kuwa amekuwa akimuomba msaada kimuziki. Bosi huyo wa Superstar Entertainment ameweka wazi tusioyajua kuhusu Parroty kwa kusema kwamba msanii huyo hajawahi walipa wasanii aliowashirikisha kwenye wimbo wake wa Lewa Remix. Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii kutia bidii kwenye kazi zao za muziki badala ya kulalamika mtandaoni.

Read More
 VDJ JONES AMVUA NGUO MADOXX WA BOONDOCKS GANG, ADAI MIHADARATI IMEATHIRI UTENDAKAZI WAKE

VDJ JONES AMVUA NGUO MADOXX WA BOONDOCKS GANG, ADAI MIHADARATI IMEATHIRI UTENDAKAZI WAKE

DJ maarufu nchini VDJ Jones amepuzilia mbali madai kuwa msanii wa Boondocks gang Edu Madoxx anapitia wakati mgumu siku chache baada ya msanii huyo kujitokeza na kuomba msaada wa kodi kutoka kwa wakenya. Katika mahojiano yake hivi karibuni Vdj Jones ambaye ni muasisi wa muziki wa gengetone amefichua tusiyoyajua kuhusu Madoxx kwa kusema kwamba madawa ya kulevya yameponza msanii huyo kiasi cha kuwafanya wasanii wenzake Exray pamoja na Odi wa Murang’a kumkimbia. Vdj Jones ameenda mbali zaidi na kusema kuwa msanii huyo amekuwa akitumia mihadarati kwa kipindi kirefu  jambo analodai limemuathiria kiafya na hata kumpelekea kuzembea kwenye suala la kufanya kazi katika kundi la Boondocks gang. Hata hivyo watumiaji wa mitandao wa kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Vdj Jones wengi wakimtaka aache suala la kutoa lawama kwa msanii huyo na badala yake ashirikiane na mashabiki wamsaidia madox ambaye wakenya wengi wamehoji kuwa huenda anapitia msongo wa mawazo.

Read More
 VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

Dj maarufu nchini Vdj Jones ametoa wito kwa chama cha uda kinachoongozwa na Naibu Rais Dakta. William Ruto kumlipa msanii Exray kwa kutumia wimbo wake wa “Sipangwingwi” kwenye kampeni zao za kisiasa. Kwenye mahojiano na Plug tv, Vdj Jones ambaye pia mwanamuziki amesema ameumizwa sana na kitendo cha wanasiasa kutumia wimbo wa sipangwingwi kujitakia makuu ilhali Exray anaishi maisha ya uchochole mtaani. Hata hivyo ametaka haki itendeke juu ya suala hilo ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Vdj Jones ambapo wametaka aache ishu ya kutumia jina la Exray kutafutia kiki. Utakumbuka mapema Exray alifunguka kuwa wimbo wake wa “Sipangwingwi” umempa mafanikio makubwa kwani wimbo umempelekea kumiliki gari.

Read More